BODABODA
mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, mwanzoni mwa wiki hii
alionja joto ya jiwe baada ya kuhenyeshwa na polisi kufuatia kitendo
chake cha kukataa kutii sheria bila shuruti, alipotaka kusababisha ajali
Barabara ya Chuo Kikuu, eneo la Mlimani City, jijini Dar.
Dereva bodaboda akidhibitiwa na polisi.
Shuhuda wa sakata hilo aliliambia gazeti hili kuwa, mwendesha
bodaboda huyo aliyekuwa akitokea Mwenge kuelekea Chuo Kikuu, alisimama
barabarani ili kuzungumza na abiria aliyemsimamisha ndipo askari wa
Jeshi la Polisi wanaotembea na pikipiki, walimfuata na kuzungumza naye.
Dereva bodaboda akipambana na polisi.
“Polisi walimuuliza kwa nini amesimama barabarani kwani kitendo hicho
kingeweza kusababisha ajali, walimtaka awape funguo kwa kile
walichosema kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria, lakini bodaboda
alikuja juu na kuanza kutaka kupambana na polisi,” alisema shuhuda huyo.
Inadaiwa kuwa baada ya polisi hao waliokuwa na silaha zao za moto,
kuzozana kwa muda bila mafanikio na bodaboda huyo, walinzi wanaolinda
lango la kuingilia Mlimani City waliungana na polisi kumtaka mwendesha
pikipiki huyo kukubali kufuata sheria.
Wakimtia nguvuni.
“Baada ya kuona askari wa pikipiki na walinzi wamemzunguka mwenzao,
bodaboda mwingine naye alisogea na pikipiki yake pale ili aweze
kumsaidia, lakini naye akajikuta akiibwaga pasipo kufanikiwa kumnasua
dereva huyo ambaye alikuwa jeuri,” alisema shuhuda mwingine.Askari hao
walifanikiwa kumtaiti mwendesha bodaboda huyo na kwenda naye kituoni kwa
maelezo zaidi.
Post a Comment