Judith Wambura ‘Jide’.
Mastaa wengi wamekuwa hawadumu kwenye ndoa zao na wengine kwenye
uhusiano wao wa kimapenzi. Ukijaribu kumuuliza kijana yeyote mwenye nia
ya kuoa atakuambia bora aoe mwanamke wa kawaida kuliko staa.
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Yobnesh Yusuph 'Batuli'.
Si suala la kuoa tu, hata kwenye mapenzi ya kawaida ni wachache
wanaoanzisha uhusiano na mastaa wakiwa na ndoto za kudumu kwa muda
mrefu. Ukiona kijana ‘anamsalandia’ staa ujue ni ili amuonje tu kisha
amtose.Pia ukifuatilia utagundua kuwa, mwanamke wa kawaida akitokea kumpenda staa wa kiume, anatafuta ile sifa ya kuwa naye lakini anajua hawezi kudumu naye.Kutokana na hilo sasa, makala haya yanajaribu kukupa kwa ufupi sababu 10 ambazo zinawafanya mastaa wengi wa kike kutodumu kwenye ndoa.
Tamaa
Hili lipo sana kwa mastaa wa kike. Baadhi yao wana tamaa ya kuwa na maisha f’lani ili waonekane nao wamo wakati uwezo haupo. Matokeo yake sasa akiolewa na mwanaume ambaye hana kitu, akimpata wa pembeni ‘pedeshee’ wa kumtunza, kwa tamaa zao hujikuta wakisaliti.
Unakuta msichana kwa kuwa ni staa, anataka awe na gari zuri, abadili nguo kila siku, simu kali na vitu vingine vya thamani wakati pesa hana na mume naye ni kapuku. Hapo ndipo wengi huamua kuchepuka na matokeo yake sasa hajali tena ndoa.
Ustaa mwingi
Mastaa wengi wakishajitambua kuwa wao maarufu, basi hata kwa wapenzi wao wanaleta zile nyodo za ustaa. Wanasahau kuwa hata rais anapokuwa na mkewe humnyenyekea kama mke na mambo mengine kuendelea.
Utakuta staa anataka kuonesha ustaa wake kwa mumewe, yaani anataka mume awe chini yeye awe juu kisa tu anatikisa jiji.
Halima Yahaya ‘Davina.
Unyenyekevu katika mapenzi unakuwa haupo, eti anajipa imani kwamba
hata akiachwa kwa kuwa anapapatikiwa na wanaume wengine kutokana na
ustaa wake, hatakosa wa kumchukua. Hiyo ni dhana potofu!Uvivu, kupenda kulala…
Baadhi ya mastaa hata wakiolewa wanashindwa kuvaa joho la ‘mke wa mtu’. Wanapenda kukaa tu na kuletewa kila kitu nyumbani. Akicheza muvi moja na kujulikana basi anaona dunia ndiyo yake, hakumbuki kutafuta kazi ya uhakika.
Usiku atapenda atoke, mchana ni mtu wa kulala tu kisa kachoka. Ni mwanaume wa aina gani atakayemvumilia?
Starehe kwa sana
Mke wa mtu hata kama anastahili kustarehe siku mojamoja, lakini baadhi ya mastaa walioingia kwenye ndoa huona wao starehe lazima ichukue sehemu kubwa ya maisha yao. Atalazimisha kila siku watoke na hata kama mume atakuwa si mtu wa kuendekeza mambo hayo, yeye ataomba awe anaenda na mastaa wenzake, akikataliwa inakuwa tatizo.
Hawajitambui
Mastaa wengi wanakosa elimu ya kujitambua. Ndiyo maana wengi wanaitwa malimbukeni. Unakuta staa amepata mume mzuri tu lakini yeye anashindwa kujitambua kuwa yeye ni mke wa mtu asiyestahili kuingiza ustaa wake kwenye maisha yake ya nyumbani.
Ndoa fasheni
Jaribu kuchunguza utagundua kuwa, mastaa wengi wanaolewa kama fasheni. Utamkuta staa wa kike anasema wazi kwamba, amechangia wengi sana hivyo na yeye anataka kuchangiwa hivyo analazimisha kuolewa.
Wanaoolewa kwa sababu hiyo ni wale ambao hata ndoa zao zikivunjika hawaoni hatari, wanaona ni sawa tu kwa sababu angalau wameonja ndoa!
Uvumilivu wa shida
Mara nyingi watu wanapooana hukubaliana kuishi pamoja kwa shida na raha. Mastaa wengi hawataki shida, wao wanataka raha tu.
Matokeo yake sasa ukiona mambo yanaenda kombo, ni wachache sana wanaoweza kuvumilia shida. Wengi wataanza visa na hatimaye wataomba talaka au kuamua kutoka kwenye ndoa!
Dhana potofu
dhidi yao
Mastaa wengi wanaonekana si watu wa kuolewa. Sasa anapotokea mwanaume wa kumuoa staa, hata kwenye mambo ya kawaida ataona anafanyiwa hivyo kwa sababu ya ustaa.Matokeo yake sasa, hata kama staa huyo atajitahidi ili adumu kwenye ndoa yake atashangaa ile damu ya ustaa inamtesa.
Wanakosa staha
Mke kama mke lazima awe na staha, kitu ambacho baadhi ya mastaa wanakikosa. Utakuta staa kaolewa lakini ana marafiki wengi wa kiume na anataka mume wake asihoji juu ya urafiki wao.Kama ni msanii akiwa lokesheni, afanyiwe lolote na wanaume, avae nguo hata za utupu kisa eti anaigiza. Mbaya zaidi si lokesheni, hata nje ya fani wanataka kuishi kisanii.
Jack Patrick.
Wako tayari kuachikaMastaa wengi wa kike wakiolewa, wanakaa mkao wa kuachika wakati wowote. Ni wachache wanaofanya jitihada za kutunza ndoa zao. Yaani wanatembea kwenye ile dhana potofu kwamba staa hawezi kudumu kwenye ndoa.
Sababu hizo hapo juu na nyinginezo ndizo zilizosababisha ndoa za mastaa kama vile Nuru Nasoro ‘Nora’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jack Patrick, Aunt Ezekiel’, Salome Urasa ‘Thea’, Halima Yahaya ‘Davina’, Judith Wambura ‘Jide’, Stara Thomas na wengineo kuvunjika
Post a Comment