JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 15, May 2015
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitishwa na taarifa za uvumi
zilizotolewa kuenea kwenye mitandao ya kijamii facebook, whatsapp na
twitter zikieleza kuwa JWTZ inafanya usaili leo tarehe 15 May
2015 katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa wale waliosoma fani ya Computer science, IT, Electronics na Mechanical Enginering.
JWTZ
linapenda kuwajulisha wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo
kuwa taarifa hizo si za kweli ni uvumi, JWTZ lina utaratibu wake wa
kuandikisha Jeshini ambapo hutoa taarifa katika vyombo vya habari kwa
utaratibu ulio sahihi.
Aidha,
Jeshi linaendelea kusisitiza wananchi kuwa halina akaunti za mitandao
hiyo na ni kinyume cha sheria kusambaza ujumbe kwa kutumia jina au nembo
ya JWTZ watakao bainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963
Post a Comment