Head of India Tanzania
Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu akiwakaribisha
wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika kwenye mafunzo
ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey Adroph wa pamoja
blog).
Afisa mipango kutoka
UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa anayeshughulikia na masuala
ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (wa kwanza kutoka kushoto)
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao kwa walimu wa
vyuo vya elimu
Ofisa anayeshughulikia
masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari akifungua mafunzo
kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO yaliyofanyika jijini
Dar.
Bi. Eunice Gachoka kutoka
Kenya Institute of Curriculum Development akijitambulisha kwa walimu
(hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya kupitia mtandao.
Daudi Mbona mkufunzi kutoka
chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu walioudhuria
mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika kwenye chuo cha Dar es
Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini Dar.
Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo.
Na Geofrey Adroph, Pamoja blog
UNESCO imeaandaa mafunzo ya
uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo
mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo
yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam
Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa
vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya
Tehama.
Hii inatokana na baada ya
mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa
nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa
na matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.
Baada ya kuona kuna mapungufu
hayo UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust
Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania
waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni
kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu
wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia
pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika
kufundishia na kujifunzia, Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo
alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta,
Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika
ufundishaji wa masomo hayo .
Kupitia mradi huo wa (CFIT),
UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu
kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi
na ufanisi katika ukuzaji wa Tehama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao
na pia kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa
matumizi ya Teknolojia
Mafunzo haya yaliyoandaliwa
na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of
Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo
ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama.
Wakufunzi wa mafunzo hayo ni
Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka
(DIT) na Godfrey Haongo kutoka Open University of Tanzania ambao
wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa .
Waalimu tisa kutoka chuo cha
ualimuTabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne
kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili
kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso
District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara
ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza
kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.
Kutokana na kuwa na uelewa
mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa
mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa
huduma za kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa
kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo
katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo
mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika
kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.
Post a Comment