WAKIMBIZI 800 kutoka nchini Burundi wameingia nchini kupitia mkoani
Kigoma huku wengine 87 wakirejeshwa nchini mwao baada ya kuingia nchini
kwa kupitia wilayani Ngara mkoani Kagera.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Isack Nantanga alisema
wakimbizi hao wameingia nchini kwa makundi madogo madogo na
watahifadhiwa kwa muda katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Akizungumza na mtandao huu jana,Nantanga alisema wakimbizi wanaofikia
800 wameshaingia nchini huku walioingia kupitia mkoani Kagera ilibidi
warejeshwe walipotoka kutokana na kukiuka sheria za kimataifa kwa
wakimbizi kuingia nchi nyingine wakivuka nchi moja.
Walianzia Rwanda.
Alisema hawapokei wakimbizi wanaotokea Rwanda kutokana na kuwa sheria
za kimataifa haziruhusu wakimbizi kuvuka nchi moja ndiyo maana
waliwarejesha wakimbizi hao.
Alisema kati ya wakimbizi hao waliopokelewa mkoani Kigoma wameingia kupitia vijijini ambapo serikali za vijiji wanawapokea na kuwahoji kisha kuwapeleka kigoma mjini kwenye kituo maalum.
Alisema kati ya wakimbizi hao waliopokelewa mkoani Kigoma wameingia kupitia vijijini ambapo serikali za vijiji wanawapokea na kuwahoji kisha kuwapeleka kigoma mjini kwenye kituo maalum.
Alisema serikali za vijiji na wilaya kwa kushirikiana na halmshauri
wamekuwa wakaifanya kazi ya kuwahoji kujua sababu hasa ya kuwafanya
wakimbilie nchini humu kwani isije kutumika vurugu za Burundi watu
kuingia nchini.
“Serikali kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa la
kuhudumia wakimbizi (UNHCR) baada ya kuwahoji na kuwapa misaada muhimu
wanaobainika kupata hifadhi wana mpango wa kuwapeleka kwenye kambi ya
Nyarugusu kwa muda,”alisema.
Msemaji huyo alisema baada ya kuhifadhiwa katika kambi hiyo mipango
inaendelea kufahamu njia nyingine za kuwahifadhi.
Kutoka Kigoma Mratibu wa idara ya wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya ndani kanda ya Magharibi Kigoma,Tonny Laiser amesema kuwa wakimbizi hao wameanza kuingia mkoani Kigoma wakipitia maeneo tofauti ya mpaka kati ya mkoa huo na nchi ya Burundi.
Kutoka Kigoma Mratibu wa idara ya wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya ndani kanda ya Magharibi Kigoma,Tonny Laiser amesema kuwa wakimbizi hao wameanza kuingia mkoani Kigoma wakipitia maeneo tofauti ya mpaka kati ya mkoa huo na nchi ya Burundi.
Wengi wa wakimbizi hao wametokea mji wa Bujumbura na wameingia Kigoma
kwa usafiri wa boti kupitia bandari ndogo ya Kibirizi mjini Kigoma.
Inaelezwa kuwa kundi kubwa la wakimbizi liliingia nchini juzi katika
mpaka wa Tanzania na Burundi kwenye kijiji cha Kagunga mwambao wa
kaskazini wa ziwa Tanganyika ambapo kundi la wakimbizi 200 waliingia
kupitia kijiji hicho.
Tayari wakimbizi 68 ambao waliingia na kufikia kambi ya muda ya NMC
kibirizi mjini Kigoma wamepelekwa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani
Kasulu ambayo kwa sasa ndiyo kambi pekee mkoani Kigoma inayohifadhi
wakimbizi.
Akizungumzia kuingia kwa wakimbizi mkoani humo Mkuu wa mkoa Kigoma,
Issa Machibya alisema kuwa wameanza kupokea wakimbizi kutoka vijiji
mbalimbali vya wilaya za Buhigwe,Kasulu na Kibondo ambao wanakimbia hali
ya machafuko nchini Burundi.
Machibya alitaja maeneo ambayo hadi sasa yamekuwa yakipokea wakimbizi
hao kuwa ni pamoja na Kijiji cha Kagunga wilaya ya Kigoma,
Muyama,Kibande na Kilelema ambavyo vyote vipo katika wilaya ya Buhigwe
mkoani Kigoma.
Kuingia kwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania kunatokana kuanza
kwa machafuko nchini humo kati ya wananchi wanaopinga kitendo cha Rais
wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza kuongoza muhula wa tatu wa uongozi
dhidi ya polisi na wanajeshi wanaomtii raisi huyo.
Kwa siku mbili mfululizo kumekuwepo na taarifa za kuchomwa mwa mabasi
mawili ya abiria na moja kulipuliwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono huku
kukiwa na vifo vya watu kadhaa kutokana na makabiliano ya waandamanaji
na polisi.
Wageni wamekuwa wakizuiliwa kuingia mji mkuu wa Burundi, Bujumbura
ambako kwa kiasi kikubwa maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunzinza
kuongoza muhula wa tatu yanaendelea ambapo kwa sasa maandamano hayo
yameanza kusambaa mikoa ya jirani na mji Mkuu wa Bujumbura.
Kwa upande wa wilaya ya Ngara, Mkuu wa wilaya ya Ngara, Costantine
Kanyasu amesema Serikali ya Tanzania imewarejesha wakimbizi 87
waliotokea Burundi kwa madai kuwa wamekimbia mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe.
Wamerejeshwa kutokana na kutofuata taratibu za kuomba hifadhi ya
ukimbizi. Aliuambia mtandao huu jana mjini Ngara kuwa kuanzia Aprili 29
mwaka huu mpaka Mei mosi waliingia wakimbizi 87 kutoka Burundi kupitia
njia za panya bila kufuata utaratibu ambapo walipokamatwa na kuhojiwa
walidai wanakimbia mapigano yanayoendelea nchini mwao.
“Tulipopata taarifa tuliwasaka na kuwakamata kisha tukawasiliana na
Serikali yao ambapo walituhakikishia usalama wa watu wao na kutuomba
tuwarejeshe nchini mwao kwa sababu hali ni shwari na sisi jana
tuliwarejesha kwao ambapo walipokelewa na uongozi wa Serikali
yao,”alisema Kanyasu.
Alisema baada ya kuwarejesha makwao hakuna taarifa nyingine za
kuonekana wakimbizi wakiingia wilayani huo kwani wananchi kwa
kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wanahakikisha kila
anayejipenyeza wanamtambua na kutoa taarifa.
Post a Comment