Waziri wa Afya afungua semina kwa waandishi wa habari kuhusu usalama wa chakula


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Seif  (kushoto), akihutubia wakati akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu usalama wa chakula. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando (kushoto), akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo.
Mkuu wa kitengo cha usalama wa  chakula  maji na usafi wa mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Stephen Kiberiti akitoa mada kuhusu rasimu ya sera ya taifa ya chakula salama  na bora katika semina hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Afya kwa Umma, Helen Semu (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Raymond Wigenge wakati wa semina hiyo. Wakurugenzi hao walikuwa watoa mada katika semina hiyo.
 
  
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando (kulia), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kinga  wa Wizara hiyo, Dk.Georgina Msemo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Raymond Wigenge(kushoto), akielekezana  jambo na Ofisa Afya Muelimishaji wa Wizara hiyo, Aggrey Mshana wakati wa Semina hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/).

Post a Comment

Previous Post Next Post