'Serikali ya Pierre Nkurunziza imepinduliwa Burundi

'Serikali ya Pierre Nkurunziza imepinduliwa Burundi'

Mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Burundi ametangaza kuwa Rais Pierre Nkurunziza amepinduliwa baada ya machafuko ya zaidi ya wiki mbili yaliyozuka baada ya Nkurunziza kuamua kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo.

Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza leo kupitia redio ya taifa jijini Bujumbura kwamba, kuanzia sasa Rais Pierre Nkurunziza si rais tena wa Burundi.

Amesema, serikali imevunjwa, makatibu wa kudumu wa mawaziri wataendesha masuala ya nchi hiyo hadi tangazo jingine litakapotolewa.

Tangazo la Meja Jenerali Niyombare limekuja baada ya jeshi la Burundi kuzizingira ofisi za redio ya taifa katika jiji la Bujumbura.

Mapema leo polisi wa Burundi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliojaribu kulivamia bunge

Post a Comment

Previous Post Next Post