
MCHUMBA wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari’ amedaiwa kuangua kilio baada ya kuvuja kwa picha yake na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mzamili Katunzi ambayo ilidaiwa kuwa ni mtu wake na kusababisha gumzo mjini.

“Zari kamaindi kweli, anajiuliza huyo aliyeivujisha alikuwa na lengo gani?” alisema mtu huyo.
Jitihada za kuzungumza na Zari hazikuzaa matunda lakini bahati nzuri Diamond alipatikana na kufafanua:
“Ni kweli zimemsumbua baby lakini nimemuweka sawa kwa kuwa najua ni mambo ya mitandao, hakuna ukweli wowote.”
ZARI, PEDESHEE KATUNZI LAIVU!
KABAAANG! Wakati supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitembea kifua mbele huku akijinasibu kuwa anasubiri kwa hamu kupata mtoto kutoka kwa mchumba wake, Zarinah Hassan ‘Zari’, imevuja picha inayomuonesha laivu mwandani wake huyo akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi ikidaiwa kuwa ni mtu wake wa nguvu, Ijumaa lina stori kamili.
Post a Comment