Kura zikihesabiwa Uturuki
Huku
kura nyingi zikiwa zishahesabiwa katika uchaguzi mkuu wa Uturuki, chama
tawala cha AK kinaonekana kupoteza idadi kubwa ya wabunge wake.
Matokeo
yanaonyesha chama hicho kimeshinda kwa asilimia arobaini na mbili ya
kura, huku kikiwa na upungufu wa viti kumi na nne kuweza kuunda
serikali.
Huku kile kinachoungwa mkono na wakurd cha HDP kikivuka
asilimia kumi kwa kupata viti takriban themanini hivyo kuweza kuingia
bungeni kwa mara ya kwanza.
Iwapo itathibitishwa, matokeo haya
yanaashiria mwisho wa utawala wa miaka kumi na tatu wa chama cha AKP
hali itakayokwaza mipango ya rais Erdogan ya kumpa rais madaraka zaidi.
Baada
ya kupiga kura yake katikati mwa Uturuki katika mji wa Konya, waziri
mkuu Ahmed Davutoglu aliongea na waandishi wa habari, na kuwaeleza
kwamba"natarajia mema kwa nchi yangu na watu wangu. Leo niko hapa kama
waziri mkuu kwa hiyo nina jukumu. Siku ya leo ni ishara ya imani ya nchi
yetu, kwa hiyo nataka kusema asanteni nyote ambao mmeshiriki katika
uchaguzi wa bila kujali uamuzi wenu."
Post a Comment