Chezea hasira za kichapo mfululizo wewe.Kocha out

 
KOCHA Mkuu waTaifa Stars , Mart Nooij akisindikizwa kutoka uwanjani chini ya ulinzi mkali wa Polisi baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu yake na Uganda, Stars walilala kwa mabao 3-0,


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika
kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya
Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania
na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.*Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;*

*1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21,
2015.*

*2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.*

*3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya
Taifa.*

*IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)*

No comments:

Post a Comment