Mheshimiwa
Samweli Sitta akitangaza nia mbele ya umati wa wananchi katika uwanja
wa Ikulu ya Unyanyembe katika manispaa ya Tabora.
Mheshimiwa Samuel Sitta leo hii alitangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitangaza nia yake hiyo mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.
Akieleza sababu tano zilizomfanya atangaze nia yake ambazo ni
1.Muungano
Toka
pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye
kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na
Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai
kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru
kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.
2. Mchakato wa katiba
Pamoja
na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini
katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza
kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa
amani.
Binafsi
naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao
wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano
kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki
saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.
3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda
Ili
kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na
huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza
huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na
maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa
uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi
zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya
ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia
hapa kwetu.
4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa
Rushwa
kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba
mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji,
uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha
hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya
kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.
5. Kuimarisha CCM kiuchumi
Chama
tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika
hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na
vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha
shughuli zake kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka
serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya
rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio
waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni "wafadhili"
Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba.
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini
Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui
Agness Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia leo
Aidha Mh Sitta akijibu swali toka kwa mwandishi wa habari aliyeuliza "Mh
Sitta unasemaje juu ya shutuma za waziri mkuu aliyejiuzuru wadhfa wake
kuwa wewe na Mh Mwakyembe mlikuwa na wivu naye ndio maana mkamuonea
mpaka ikabidi ajiuzuru? Mh Sitta akajibu "Bwana mwandishi kwa nini swali hilo humuulizi yeye mwenyewe aseme ni kipi alichoonewa? Mchakato wa uchunguzi ulifanyika mwaka 2008 mpaka
sasa ni miaka 7 hivi sasa muda wote huu alikuwa wapi hata leo aseme
alionewa? Jibu ambalo lilipelekea vicheko na vigerere toka kwa wananchi
walioudhuria hafla hiyo.
Mtemi
wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira akiwatambikia Mh Magreth Sitta
na Mh Samuel Sitta ambaye ni binamu yake kabla hajatangaza nia ya
kugombea urais.
Picha na Habari na Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE
Post a Comment