Nassari atumia Helikopta kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura jimboni kwake


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akisalimiana na rubani wa Helkopta wakati anaanza ziara ya kuhamaisha zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR.
Mbunge Nassari akifunga mikanda tayari kwa kuanza ziara.
Mbunge Joshua Nassari akiteremka kutoka katika helkopta wakati alipofika katika kata ya Shambalai Burka kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamembeba Mbunge Joshua Nassari mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Shambarai Burka.
Mbunge Joshua Nassari akisalimiana na mmoja wa watoto waliojitokeza kumpokea.
Kundi la kina mama pia walikuwa miongoni wananchi waliojitokeza kumpokea Mbunge Nassari.
Mbunge Joshua Nassari akiwa na viongozi wengine wa Chadema wilaya ya Arumeru.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arumeru ,Gadiel Mwenda akizungumza katika mkutano uliofanyika kata ya Shambarai Burka kuhamasisha wanachi kujitokeza katika zoezi la uandikishwaji.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassar akizungumza na wananchi katika kata ya Shambarai Burka wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
Mbunge Nassari pia alitumia mkutao huo kuwaonesha wananchi magari mawili ya kubeba wagonjwa aliyotoa kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Arumeru.
Magari mawili ya kubebea wagonjwa yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya watu wa jimbo hilo.
Mbunge Nassari akiwaapisha wananchi ikiwa ni moja ya hamasa kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Mbunge Nassari akiondoka katika uwanja huo mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

Post a Comment

Previous Post Next Post