
Omotola Jalade , nyota wa filamu wa Nigeria ambaye
amefikisha miaka 20 katika tasnia hiyo na kuwa alama ya fahari ya tasnia
ya filamu ya Nollywood ya Nigeria, ametoa ya moyoni kuhusu
kinachomfanya asitetereke kwenye ndoa yake ambayo imempatia watoto
wanne.

Kipenzi huyo cha mamilioni ya wapenda filamu duniani, akijulikana kwa
jila la utani la Omosexy, amesema mumewe, Kapteni Mattew Ekeinde,
ndiye kila kitu kwake na kwamba ndiye mtu pekee anayeweza kumdhibiti.
“Sidhani ningekuwa nimeolewa hadi sasa kama nisingeolewa mapema,
kwani naona hakuna mtu awezaye kunidhibiti zaidi ya mume wangu. Si
kwamba mimi ni mkorofi, bali nina msimamo imara. Sifahamu nini
kinawafanya wasanii wengine wa kike kutopata wanaume sahihi wa kuishi
nao,” alisema katika mahojiano hivi karibuni na gazeti la Vanguard.
Alisema wasanii wanapopata mafanikio wanachanganyikiwa na kushindwa
kufahamu watu wanaowapenda kwa dhati kwa vile wanajiona wako matawi ya
juu. Hii huwaletea matatizo wao wenyewe.“Mimi nimebarikiwa, nimefanya
uamuzi wa makusudi bila kumwathiri mtu mwingine. Ni kwa vile ni uamuzi
wa asili. Nina bahati kwa vile Mungu alinifundisha jinsi ya kutumia
akili yangu,” alisisitiza mwigizaji huyo.
Post a Comment