WAKATI
ikiwa imebaki miezi minne tu ili kufikia tarehe ya Uchaguzi mkuu wa
Urais,wabunge pamoja na Madiwani hapo Octoba 25 mwaka huu,sasa Vyama vya
Upinzani vya ACT-Wazalendo pamoja
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema vimeingia tena kwenye
Uhasama mkubwa ambao unaweza ukavivuruga vyama hivyo.(Mtadandao huu
unaripot)i.Anaandika KAROLI VINSENTendelea nayo
Ni Baada ya leo Chama cha ACT –wazalendo kusema wamepanga
kukifanyia kitu kibaya chama cha Chadema ambapo wanadai Viongozi wa
Chadema hawatakisahau maishani mwao.
Hayo yamesemwa Mda huu Jijini Dar Es Salaam na Katibu wa
Mipango na Mikakati Taifa wa ACT-Wazalendo Habibu Mchange ,wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari ambapo Mchange amesema kwa sasa chama
hicho kimechoka na kitendo wanachodai kinafanywa na Chadema cha kuwakodi
watu kuja kufanya fujo kwenye mikutano yao.
“ Sisi tumebaini wazi kwamba chadema wanawakodi watu na kuja kufanya
fujo kwenye mikutano yetu tumeona kule Tunduma mkoani mbeya na hata huyo
Kionngozi wao Mnyika ametangaza kuwa sisi ni Adui basi wakiendelea
,tutawafanyi jambo baya sana na litakalokimaliza kabisa chama
hicho,Amesema Mchange.
Habibu Mchange ambaye anawania Ubunge kwenye Jimbo la Kibaha
Mjini Mkoani Pwani kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi mkuu wa hapo
baadae mwaka huu amebainisha kuwa kwa kusema anaifahamu Chadema licha
ya kuwa huko, kwani hawawezi kumtisha na atakavyowafanyia jambo baya
hilo,anadai atatumia njia nyingi.
“Mimi Chadema naijua kwani mimi ndio niliyoijenga chadema mpaka kufikia
hapo,kama hamjui mimi ndio niliyotengeneza mipango kama ya “Movement
For Change” (M4C),Oparesheni Sangara,mimi ndio nilioijenga
Chadema,kwahiyo hata hao wakina Dk Slaa na Mbowe wake hawawezi kufanya
hivyo nawaambieni, hawezi kunipa shida kuwafanyia jambo baya,waendeleea
waone”amebainisha Mchange..
Wakati huo huo Chama cha ACT-Wazalendo kimewataka kupita viongozi wake,
kimewataka Wananchi na wanachama wa chama hicho mkoani Dar es Salaam
kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa utakao fanyika Viwanja vya
Mwembe Yanga vilivyopo Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam siku ya
Jumamosi ya Julai nne mwaka huu.
Ambapo kwa mujibu wa Mchange amesema Mkutano huo mkubwa ambao utarushwa
(live)yaani moja kwa moja kupita Vituo vya TV na Redio unatajwa kuwepo
na Ajenda mbali mbali jambo analo anadai litakuwa linalengo la kumkomboa
mtanzania wa leo.
Post a Comment