
KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ameupongeza uongozi wa
Simba kwa kumrejesha Mwinyi Kazimoto akisema atarejesha ufalme wa klabu
yao Bara.
BADO WEWE => INGIA HAPA(MAISHA TANANIA)
BADO WEWE => INGIA HAPA(MAISHA TANANIA)
Mkude alisema: “Tulikosa kiungo mzoefu na mwenye
uwezo kama wa Kazimoto, ni muda wetu sasa kulitawala soka la Tanzania.
Nimesikia juu ya ujio wa Kazimoto, bado sijamuona kambini lakini kama
kuna kitu kikubwa walichofanya uongozi ni kumrudisha fundi Kazimoto.
“Tangu alivyoondoka, sikuona aliyeweza kufunika
kazi yake, mimi binafsi naamini sijaweza kuufikia ubora wake, lakini
sasa naamini anakuja na vitu vipya ukizingatia kuwa ana uzoefu mkubwa na
amecheza soka nje.
“Hivi karibuni nilicheza naye kwenye Taifa Stars,
kiukweli yuko vizuri sana hata kuliko vile alivyokuwa kabla ya kuondoka
Simba.”
Kiungo huyo pia amebainisha kuwa kwa usajili uliofanywa msimu huu ni lazima kila mchezaji ajitume ili ajihakikishie namba.
“Usiwaone akina Kiiza (Hamis), Mgosi (Mussa
Hassan) na wengine wote wageni, wako vizuri sema tu kwa sasa mchezaji
kupata nafasi kwenye kikosi ni rahisi na hauhitaji kutumia nguvu nyingi
kama ilivyokuwa hapo nyuma wakati timu ilipokuwa na viungo kama kina
Kazimoto, Haruna Moshi ‘Boban’ na marehemu Mafisango (Mutesa).
Kiiza
Mshambuliaji Hamis Kiiza amekiri kinachofanywa na
Simba kwa sasa hakuwahi kukiona hata Yanga na kudai kuwa uwepo wa kocha
wa viungo Simba utafanya kila mchezaji awe staa kwani kila mmoja lazima
awe na kiwango bora.
Kiiza ambaye ni raia wa Uganda alisema:
“Nisikufiche, nilivyokuwa Yanga kilichonipa umaarufu ni uwezo wangu na
kujituma kwangu lakini uwezo wangu mkubwa ulichangiwa na kocha wa
viungo.
“ Pale Yanga hakukuwa na kocha wa viungo ingawa
mimi binafsi nilikuwa na kocha wangu ambaye nilikuwa nikimlipa mwenyewe
ili niwe fiti na hicho ndicho kilichonijengea jina.
“Kwa hali hii ya Simba naamini sasa kila mchezaji
atakuwa staa na atakuwa na jina kubwa kutokana na uwezo atakaokuwa nao
uwanjani.
“Kama kuna kitu Simba itakuwa imezipiga bao klabu
zingine kwanza ni kuwa na mtaalamu wa viungo lakini pia itakuwa na
wachezaji wengi wenye uwezo wa ajabu.
- Mwanaspot
- Mwanaspot
Post a Comment