Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa inaongeza muda wa siku nne tu
wa kuandikisha wapiga kura kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Hii
inamaanisha kuwa zoezi hilo ambalo lilikuwa linaisha ijumaa ya kesho
julai 31, litaendelea hadi jumanne agosti 4
Akiongea
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC,
Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi
ya siku nne kwa kuwa ratiba zitaingiliana.
Aidha,
Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka sasa watu zaidi ya milioni 18
wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya mfumo
wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima.
Post a Comment