Vituko vya Maradona haviishi!! safari hii kamtuhumu mke wake kumwibia fedha

maraa
Mkongwe wa soka duniani Diego Maradona amerudi kwenye headlines tena baada ya kumtuhumu mke wake wa zamani Claudia Villafane kuwa amemuibia fedha kwenye akaunti yake.
Maradona akizungumza kwenye matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni alisema Villafañe ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani ni mwizi na amemwibia kiasi cha dola milioni 9 benki.
Hata hivyo Villafañe amepinga vikali madai hayo na kudai kuwa yeye si mwizi na hakuiba fedha hizo huku akitetewa pia na watoto wake Dalma na Giannina kwenye mtandao wa twitter.
wawil
Maradona akiwa na mke wake Claudia
Wapenzi hao ambao walikutana miaka ya zamani katika mji uliokithiri kwa umasikini huko Buenos Aires kabla ya Maradonna kuwa maarufu na kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani katika historia ya soka,waliachana baada ya kutofautiana.
Watoto wao wawili Dalma and Giannina,wamekaririwa kwenye mtandao wa twitter wakimtetea mama yao wazi wazi na kwamba hahusiki na upotevu huo wa fedha za baba yao

Post a Comment

Previous Post Next Post