WADADA WA NAMNA HII NI SHIDAAH KUWA NAO KIMAHABA


Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..
1.Demu wako wa zamani Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu,ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.
2.Dada wa rafiki yako kipenzi Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

Post a Comment

Previous Post Next Post