Breaking News: Jeshi la Polisi Lakanusha Kupiga Marufuku Maandamano ya Kumsindikiza Kuchukua fomu Mgombea urais Chadema,Edward Lowassa


Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar  es  Salaam Suleiman Kova amekanusha  kupiga marufuku  maandamano  ya  kumsindikiza  Lowassa  Kuchukua  fomu ya  kugombea  urais  ofisi  za  tume  ya  taifa  ya  uchaguzi.

Kova amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yale yanayo anzia ofisi  za  CHADEMA kwenda NEC,lakini ya kutoka Nec kwenda makao makuu ya CUF Buguruni hawayatambui.
Katika  Hatua  nyingine, Mwenyekiti  wa  CHADEMA,Freeman  Mbowe  amesema  hawana  taarifa  yoyote  ya  zuio  la  maandamano  toka  jeshi  la  polisi.
Mbowe  amesisitiza  kuwa  maandamano  ya  kumsindikiza  Lowassa  NEC  yako  palepale  na  amewataka  wapenzi  na  wafuasi  wa  UKAWA  wasiogope.

Post a Comment

Previous Post Next Post