Gundu? Miezi kadhaa baada ya kumwagana na mzazi mwenziye Siwema Edson
baada ya kumfuma na ‘kiserengeti boy’, staa wa Bongo Fleva, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anadaiwa kunyang’anywa tena mrembo wake wa
Bongo Movies, Shamsa Ford na kibabu anayedaiwa kumnunulia mwanadada huyo
gari aina ya Toyota Noah.
Habari hiyo ya mjini kwa sasa inaeleza kuwa mzozo wa Nay na Shamsa ulianza hivi karibuni baada ya Nay kudaiwa kumshtukia Shamsa akiwa na gari hilo jipya wakati yeye hakumgharamia hata senti tano.
Chanzo cha ‘ubuyu’ huo kilidai kwamba, Nay alijikuta akiingia kwenye majonzi mazito baada ya wajanja wa ‘tauni’ kumwambia kuwa Shamsa anatoka na kibabu huyo ambaye ni kibosile serikalini na tayari ameanza kuwekeza kwa kumnunulia Noah.
“Jamani ifike kipindi tumhurumie Nay maana kinachomkuta si cha kuchekelea. Hata kama ungekuwa baunsa kiasi gani lazima uwaze hasa unapojikuta ukiibiwa kila mwanamke unayetangaza kuwa naye tu.
“Juzikati niliongea na Nay, japokuwa alikuwa akichekacheka lakini ukweli ni kwamba ana machungu baada ya kugundua kuwa Shamsa kahongwa gari na kibabu.
“Kinachomshangaza Nay ni kusikia Shamsa amenunua Noah kupitia malipo ya filamu lakini ukweli ni kwamba gari hilo kahongwa,” kilisema Chanzo hicho.Baada ya gazeti hili kupenyezewa mchongo huo lilimtafuta Nay na kumsomea ishu nzima ambapo alisema kwa sasa hayupo kimapenzi tena na Shamsa zaidi ya kuwasiliana kawaida.
Kuhusu gari alisema ni kweli Shamsa ana Noah isipokuwa hajui kaitoa wapi zaidi ya kusikia kuna mtu kamhonga.
Shamsa alipofikishiwa mashitaka hayo alisema gari hilo amelinunua kwa fedha zake, hivyo Nay asiwe na hofu.

Post a Comment