JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 26.08.2015.
• MTOTO WA MIAKA SITA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
• MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
• JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WAKIWA NA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO
MWENYE UMRI WA MIAKA SITA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGNES SHOMBE MKAZI
WA CHIMBUYA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI AINA YA
TOYOTA HAICE AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.08.2015 MAJIRA YA SAA 13:10 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA AJALI. UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA JIJINI DSM ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IDD MKWACHU (41)
ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA YENYE NAMBA ZA
USAJILI T.632 DEM AINA YA TOYOTA R4 KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO
KATIKA BARABARA YA MBALIZI/MKWAJUNI MKOANI MBEYA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 25.08.2015 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA ILOLO, KIJIJI CHA NJELENJE, KATA YA SONGWE, TARAFA
YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBALIZI/MKWAJUNI.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, DEREVA WA GARI HIYO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
AHIMIDIWE NGILANGWA (29) MKAZI WA JIJINI DSM NA ABIRIA WENGINE WAWILI
WANAUME WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA.UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEGONGA NA KUKIMBIA AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI WA NAKONDE
NCHINI ZAMBIA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
ERICK SIMWANZA (18) MKAZI WA NAKONDE-ZAMBIA 2. CHARLES SILAVU (25) MKAZI
WA NTINDI – NAKONDE ZAMBIA 3. GWAKISA MWAMBOMA (30) MKAZI WA MTAA WA
MWAKA TUNDUMA NA 4. PRINCE CHISALA (27) MKAZI WA NTINDI –NAKONDE-ZAMBIA
WAKIWA NA BHANGI KETE 575.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI MAALUM ILIYFANYIKA MNAMO TAREHE
25.08.2015 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO MPAKANI KATI YA TANZANIA
MTAA WA TUKUYU [BLACK] NA NAKONDE –ZAMBIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment