Hakuna deni halali la Walimu ambalo halijalipwa - Serikali

Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akizungumza na waandishi wa habari na kushoto ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohammed Mtonga.
SERIKALI imesema kwamba imeshalipa madeni ya walimu ya kiasi cha Sh. bilioni 5.7 ambayo yaligungulika kihalali kati ya Sh. bilioni 19.6 zilizokuwa zinadaiwa kudaiwa,hivyo kwa sasa hakuna malalamiko mwalimu ambaye hajalipwa.

Aidha Serikali imependekeza kwamba halimashauri zilizowasilisha madeni ambayo si halali, yenye shaka, au watumishi wasio na madai, madai ya watumishi wasio na madai, madai ya watumishi waliokwishalipwa na waliowasilisha madai ya mishahara kama madai yasiyo ya mishahara wawajibishwe.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Likwelile alisema hayo wakati akitoa taarifa ya uhakiki wa madeni ya walimu wa shule za msingi, sekondari na Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Alisema awali wizara yake ilipokea madai ya walimu kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (WEMU) yenye jumla ya Sh. bilioni 19.6 ikiwa Sh. bilioni 17.4 kutoka TAMISEMI na Sh. bilioni 2.1 kutoka WEMU.

“Madeni ambayo hajalipwa ni kwa sababu hakuna kielelezo juu ya madai hayo,” alisema Dkt. Likwelile .

Aliongeza kwamba wizara yake kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali, ilifanya uchambuzi wa awali kwa lengo la kujiridhisha na takwimu zilizowasilishwa na TAMISEMI kwa kila halimashauri na kwa watumishi wa WEMU, ambao umeonesha kuwa na shaka na baadhi ya madai.

“Baada ya uchambuzi wa awali idara iliandaa hadidu za rejea kwa lengo la kufanya uhakiki wa madai yaliyowasilishwa. Uhakiki huo ulifanywa na wakaguzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na timu ya wakaguzi wa ndani chini ya usimamizi wa idara hiyo.

“Matokeo ya uchambuzi wa awali yalipelekea madai ya walimu na watumishi yasiyo ya mishahara kupungua kutoka Sh. 19.6 hadi kufikia Sh. bilioni 16.2.,” alisema.

Alifafanua kwamba madai hayo yaliyohakikiwa yalihusisha walimu 16,315 kutoka halimashauri 147 na watumishi, 1,152 kutoka WEMU. Madai yasiyohakikiwa ni Sh. bilioni 3.3 yakihusisha walimu 1,448 ambao hawakuwa na cheki namba na walimu 1,834 ambao cheki namba hazikuonekana kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya utumishi wa Serikali.

Dkt. Likwelile alisema kazi ya uhakiki katika halimashauri na WEMU ilifanyika kuanzia Machi 12, mwaka huu hadi Aprili 11, mwaka huu.
Aliongeza kwamba matokeo ya uhakiki yameonesha kiasi cha Sh. 5.7 kimekubaliwa na kiasi kilichokataliwa ni Sh.bilioni 10.5.

“Zoezi hili la uhakiki wa madai limeiwezeshha Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na iwapo malipo yangefanyika bila kufanya uhakiki,” alisisitiza.

Alizitaja baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni kuendelea kuwepo kwa madi ya muda mrefu kwenye halimashauri , baadhi ya madai kuwasilishwa kama madai ya mshahara, kutokuwepo kwa kumbukumbu za madai kwenye majalada ya watumishi, majalada ya walimu kutopatikana na hivyo baadhi ya madai kutohakikiwa.

Changamoto nyingine ni baadhi ya madai yaliyokwisha kulipwa kuwasilishwa kama madai mapya na baadhi ya madai kuwasilishwa zaidi ya mara moja kwa madai yanayofanana.

Akitolea mfano wa madai hayo Mkaguzi wa mifumo ya kompyuta kutoka wizra hiyo alisema yupo mwalimu aliyekuwa akidai Sh. milioni 500, wakati deni sahihi ni Sh. laki tano.

Post a Comment

Previous Post Next Post