Na Exaud Msaka Habari
Katika
kuonyesha kuwa
wapo karibu na vijana wa kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi
na
kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA
Radio 5 kimenzisha mchato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa
kitanzania
mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la
kuhakikisha kuwa
wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo na ndoto zake
Radio 5 imekuwa na
michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti
zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku
ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni
hapo kuomba saport ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani
nyingine.
Mchakato ambao sasa
unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es
salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza
darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili
waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
Katika zoezi hilo
vijana walitakiwa kutuma nyimbo zao radioni ikiwa ni pamoja na kujiandikisha
majina yao ili siku waandaaji hao watakapofika katika mtaa waliopo basi waweze
kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,na kupatikana washindi ambapo mchakato
huo utapita katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam na mwisho kuwapata
washindi wanne ambao ndio watakaoibuka na zawadi kabambe.
Lengo kuu la mchakato
huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo mtaani kutokana na sababu
mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji hivyo ambapo RADIO 5 wameamua
kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa vijana hao wanapata nafasi ya
kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa watanzania.
Msaanii maarufu wa music wa Uswazi Msaga Sumu maarufu kama Mfalme wa mtaani akitoa burudani wakati wa mchakato huo uliofanyika jijini Dar es salaam |
Wakati zoezi hilo
likiendelea mtandao huu ulipata nafasi ya kuzngumza na mkurugenzi wa RADIO 5 Bw
ROBERT FRANCIS ambaye amesema kuwa ni jambo jema kuona kazi hilo imeanza kwa
amani na furaha hivyo watanzania waendelee kuwaunga mkono huku akiwataka vijana
mbalimbali wenye vipaji mkoani Dar es salaam kuendelea kujitokeza maeneo
mbalimbali ambapo ziezi hilo litakuwa linafanyika pamoja na kuendelea
kusikiliza Radio hiyo.
Naye meneja vipindi wa
RADIO 5 Ndugu MATHEW PHILIP Akizungumza na mtaandao huu wakati zoezi hilo
likiendelea amesema kuwa kupitia vipindi vya Radio hiyo hasa vipindi vya
kutafuta vipaji nyumba kwa nyumba Dar es salaam vijana wataweza kuinua vipato
vyao huku akisisitiza kuwa watanzania waendelee kusikiliza RADIO 5 kwani kuna
mambo mengi na mazuri yanaendelea kuwajia.
Umati wa watanzania waliojitokeza kushugudia vipaji vikionyesha uwezo Jukwaani |
Meneja biashara wa
kituo hicho cha Radio Bi ANGELA MAINA alisema kuwa maana halisi ya kufanya
zoezi hilo ni kuwapa vijana nafasi ili kukuza vipaji vyao hasa katika tasnia ya
music ili miaka ijayo watanzania waone matunda ya kazi hiyo haswa kwa washiriki
wa zoezi hilo.
Aidha meneja masoko na
mahusiano wa RADIO 5 Bi SARAH LAZARO alisema kuwa pamoja na lengo kuu la
mchakato huo ni kuvumbua na kunyanyua
vipaji lakini pia ni nafasi kwa wadau wa biashara na mashirika binafsi haswa
yanayojihusisha na maswala ya kijamii kuanza sasa kushirikiana na radio 5 ili
kukuza biashara zao na kushiriki katika kuendeleza jamii.
Katika mchakato huo
endelevu utakao fanyika katika jiji la Dar es salaam unataraji kuwapata
washindi wanne wa mkoa huu ambapo washindi hao watajinyakulia zawadi mbalimbali
kama ifuatavyo
Mshindi wa kwanza
anataraji zawadi ya kurekord albam nzima bure kwenye studio za kisasa na kupata
promotion kubwa ya kazi yake,mshindi wa pili anataraji kurekord nyimbo mbili
bure pamoja na pamoja na promotion ya miezi sita(6),mshindi wa tatu atapata
kurekord nyimbo moja pamoja na promotion ya miezi mitatu,huku mshindi wan ne ataweza
kurecord nyimbo moja pamoja na promotion ya mwezi mmoja.
IMEANDALIWA NA EXAUD
MSAKA HABARI-HABARI24 BLOG
Picha zaidi nimekuwekea hapo chini
Post a Comment