Kiungo chipukizi wa Barcelona, .
Na Rabi Hume
Kocha
wa klabu ya Barcelona, Mhispania Luis Enrique amemtaja kiungo
anayechupukia katika kikosi chake Sergi Roberto, 23 kama Zinedine Zidane
mpya kutokana na aina ya uchezaji wake.
Enrique
amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Hispania
maarufu kama Primera Division uliyoikutanisha timu yake ya Barcelona na
klabu ya Getafe na Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa bila,
magoli yakifungwa na Luis Suarez na Neymar Jr.
Enrique
amesema Roberto amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi chake kutokana
na kutimiza majukumu anayokabidhiwa na mwalimu pamoja na aina yake ya
uchezaji hali inayomfanya aone kama Zidane, Pele na Diedo Armando
Maradona wakiwa ndani ya mtu mmoja ambaye ni mchezaji wake Roberto.
Kocha
huyo amemtaja Roberto kama aina ya mchezaji ambaye unaweza kumpanga
kwa aina yoyote ya mfumo unaoutumia kama acheze kushoto, kulia au hata
katikati na bado anazidi kuwa bora katika nafasi hizo.
Kocha wa Barcelona, Luis Enrique.
Aidha
Enrique alimtaja kama Robert kama moja ya wachezaji wake bora kwa sasa
katika kikosi chake kutokana na kuzungukwa na wachezaji bora wenye
viwango bora duniani kama Sergio Busquets, Ivan Rakitic na Andres
Iniesta.
“Amekuwa
mchezaji mkubwa katika kikosi chetu cha Barca na amekuja na vitu vingi
ambavyo vimefanya kikosi chetu kizidi kuwa bora pia kikichochewa na aina
ya wachezaji wanaomzunguka Segio, Rakitic na Iniesta ambao wote wana
uwezo bora zaidi,” alisema Enrique
Akizungumzia
nafasi ya mchezaji huyo kwa siku za mbeleni amesema ataheshimu maamuzi
yake lakini ni mchezaji muhimu kwa Barcelona.
Sergi
Roberto ni moja ya wachezaji ambao wamekulia katika timu hiyo na mpaka
sasa katika michezo 11 ambayo amepata nafasi ya kucheza amefanikiwa
kutoa pasi za magoli 3 akilingana na Neymar pamoja na Lionel Messi
ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Post a Comment