
Akiongea
katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkwasa amesema wamejiandaa
kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo, wanajua Algeria ni
miongoni mwa timu bora Afrika, lakini hilo halitawazuia kuibuka na
ushindi.
“Katika
mpira wa sasa duniani hakuna timu kubwa wala timu ndogo, lolote
linaweza kutokea, sisi tuna nafasi ya kufanya vizuri tukiwa katika
uwanja wa nyumbani na washabiki wetu” alisema Mkwasa.
Aidha
Mkwasa alisema wamefanya mazoezi kwa pamoja kwa takribani siku 10,
vijana wapo katika hali nzuri, hakuna majeruhi vijana wote wapo katia
hali nzuri na timu imefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya
kushuka dimbani kuwakabili Mbweha wa Jangwani.
Mwisho
Mkwasa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuja
kuwapa sapoti vijana watakapokuwa wanapeperusha bendera ya Tanzania.
Mechi kati ya Tanzania dhidi ya Algeria kesho Jumamosi itaanza saa 10:30 jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dares salaam.
MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MUSONYE

Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma
salamau za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye
kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Theresia Musonye kilichotokea leo
asubuhi katika mji wa Kakamega nchini Kenya.
Katika
salamu zake, Malinzi amempa pole Musonye na kusema kwa niaba ya familia
ya mpira wa miguu na watanzania wote, wako pamoja nae katika kipindi
hiki cha kigumu cha maombelezo na kuwapa pole ndugu,jamaa na wafiwa
wote.
Bi Theresia Musonye amefariki akiwa na umri wa miaka 77, taarifa zaidi na taratibu za mazishi zitatolewa na familia ya marehemu.
Post a Comment