Kocha wa Klabu ya Chelsea, Jose Mourinho.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Chelsea, Oscar.
Na Rabi Hume
Hali
ya mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya nchini Uingereza, Klabu ya
Chelsea sio nzuri kwa msimu wa 2015/2016 kufuatia kuanza msimu huu
vibaya kwa kuambulia points 11 katika michezo 11 iliyocheza mpaka sasa
na kukamatilia nafasi ya 15 hali ambayo inamuweka katika kipindi kigumu
kocha wa timu hiyo, Mreno Jose Mourinho.
Hilo
limethibitishwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu
hiyo ya Chelsea, Oscar ambaye amesema hali ya kocha wake Mourinho
imekuwa sio nzuri katika klabu hiyo kufuatia kipigo cha goli 3 kwa 1
walichokipata wikiendi hii dhidi ya mahasimu wao Liverpool mchezo
uliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Oscar
amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mtandao wa klabu ya
Chelsea na kuelezea kuwa kabla ya mchezo huo wachezaji pamoja na
mashabiki wa Chelsea walikuwa wakim-support kocha Mourinho lakini baada
ya mchezo huo kumalizika hali imekuwa tofauti jambo lililofanya hali ya
kocha huyo kuzidi kuwa mbaya ndani ya timu hiyo.
Mshambuliaji
huyo ameongeza kuwa wachezaji wa timu hiyo pamoja na mashabiki wa timu
hiyo wamekuwa wakijaribu kumsaidia kocha huyo ili kuweza kupata matokeo
mazuri lakini matokeo yanakuja tofauti lakini wanachopaswa kufanya kwa
sasa ni kupata matokeo mazuri.
“Kila
mtu alijaribu kumsaidia (Mourinho) lakini hali sio nzuri kwa Mourinho
kwa wachezaji na hata kwa mashabiki wa Chelsea, tunahitaji kuanza
kushinda tena,” Oscar aliuambia mtandao huo.
Akiuzungumzia
mchezo wa Liverpool Oscar amesema kuwa ulikuwa mchezo mzuri kwa upande
wao katika kipindi cha kwanza lakini hali ilikuwa tofauti hasa baada ya
mshambuliaji wa Liverpool, Phillipe Countinho kusawazisha goli la kwanza
katika dakika za mwisho za kipindi cxha kwanza za mchezo huo.
Ameongeza
kuwa katika kipindi cha pili wapinzani wao walikuja vizuri zaidi
walijitahidi kuwazuia lakini walikuwa vizuri zaidi na kumwelezea,
Mbrazil mwenzake anayekipiga Liverpool, Countinho kama nyota wa mchezo
huo aliyefunga goli la pili kwa upande wa Liverpool kabla ya Christian
Benteke kuongeza goli la 3 nala ushindi kwa Liverpool.
Post a Comment