Lilipofikia dili la Mbwana Samatta kwenda Ulaya January 2016, hii ndio kauli ya meneja wake …



Usiku wa December 24 ulikuwa ni usiku ambao zilizagaa au kuvuja habari za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta kutajwa kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Stori zilianza kama tetesi na baadae mmoja kati ya mitandao ya Ulaya ikaripoti mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya KRC Genk Dimitri De Conde kuwa katika mipango ya kukamilisha usajili huo, December 24 kunatajwa kuwa kulikuwa na mazungumzo ya kina kati ya viongozi wa KRC Genk na mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi juu ya dau la uhamisho wa staa huyo.
501184166
December 25 Jamal Kasongo ambaye ni meneja wa Mbwana Samatta amethibitisha mazungumzo kufanyika na kuwa katika hatua nzuri “Moise Katumbi jana alikuwa Ubelgiji kushughulikia hili suala lakini amerudi Lubumbashi na kumuacha mwanasheria wake aendelee nalo, kwa sasa wanavutana kuhusu ada ya uhamisho anayohitaji Katumbi ila kama wakikubaliana tumuombee mungu tu kijana January atacheza Ubelgiji” >>> Jamal Kasongo

Post a Comment

Previous Post Next Post