Tajiri wa makontena abainika


#Habari:Watu kumina mbili wamepoteza maisha na majeruhi kumina nane wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya iramba,baada ya basi la TAKBIR walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Geita kugongana na malori mawili katika kijiji cha Kizonzo mpakani mwa wilaya ya Igunga na Iramba mkoani Singida.Mganga wa wilaya ya iramba daktali Timoth Sumbe amesema wamepokea maiti kumi na mbili kati ya hizo wamo wanawake watatu,wanaume sita na watoto wa tatu huku majeruhi kumina nane wakiendelea kupatiwa matibabu ambao wengi wao wamevunjika miguu , mikono na majeraha usoni.
Posted by ITV Tanzania on Wednesday, December 2, 2015

    Ni mfanya biashara ya vipuri vya magari Kariakoo Dar
    Akubali yaishe, amtupia lawama wakala wake
    Ofisa afichua ‘dili’, mipaka hatari kwa wizi ni Burundi, Sudan Kusini

MIONGONI mwa wafanyabiashara waliohifadhi makontena yenye utata katika malipo ya kodi kwenye Bandari ya Nchi Kavu (ICD) ya mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakheresa, ni Nassoro Ahmed bin Slum, tajiri muagizaji na muuzaji wa vipuri vya magari.
Katika mazungumzo yake na gazeti hili la Raia Mwema, tajiri huyo ambaye kampuni yake inaitwa BINSLUM TYRES LTD, ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, amekiri kuwapo katika utata wa kukwepa kodi, lakini akimtupia lawama wakala wake.
 

Ingawa bin Slum, tajiri mwenye makao yake ya kibiashara Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, anasema anayo makontena zaidi ya 20, lakini taarifa za gazeti hili kutoka vyanzo vyake vya uhakika vya habari vya gazeti hili, zinaeleza kwamba anayo makontena yasiyopungua 200 ICD ya Bakheresa.
 

Bin Slum anaibuka ikiwa ni siku chache tu tangu Waziri Mkuu wa Awamu ya Tano, Majaliwa Kassim Majaliwa, kufanya ziara ya ghafla katika Mamlaka ya Bandari (TPA) Dar es Salaam na kubaini upotevu mkubwa wa mapato ya serikali, baada ya makontena ya bidhaa mbalimbali zaidi ya 349 kuondolewa bandarini hapo kinyemela bila kulipiwa kodi na hivyo kusababisha hasara ya shilingi bilioni 80.
 

Katika tukio hilo, Waziri Mkuu aliwasimamisha kazi baadhi ya maofisa wa TRA na kisha, baadaye jioni hiyo ya Novemba 29, Rais Dk. John Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade.
 

Kauli ya Bin Slum
Katika maelezo yake kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwake, Bin Slum alisema; “Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa moja kwa moja kodi serikalini, tunalipa kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali.
 

“Tunamfuata wakala, mimi nilimpa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nafanya naye kazi kwa miaka zaidi ya 10. Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi, lakini kwenye mzigo huu wa sasa ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo nami nilimdai nyaraka…akaniambia ananitayarishia faili.
 

“Baada ya hapo nikapata safari, niliporudi naye akawa kasafiri, sikuweza kumpata hata kwenye simu. Mimi nilimlipa wakala wangu hela yote ya kodi iliyohitajika sasa kama amenichezea ‘game’ ndio nataka kujua. Kipindi cha nyuma chote miaka zaidi ya 15 nimefanya naye kazi vizuri, kwa nini iwe sasa.
 

“Ningekuwa nataka kufanya wizi au nisingetumia jina langu halisi kufanya uchafu unaotajwa sasa, nipo tayari kutoa ushirikiano ili hatmaye nijue kontena zangu zilitolewa kwa njia gani,” alisema bin Slum.
 

Hata hivyo, alipoulizwa ni kwa nini aliruhusu kupokea makontena bila nyaraka halali za malipo ya kodi na alikuwa na makontena mangapi na ni nani hasa ndiye wakala wake; alijibu; “Ni kontena zaidi 20. Wakala wangu ni Kampuni ya Regional Cargo, ambaye mmiliki ni Mohammed Ally.”
 

Akaendelea kujieleza; “Nina majanga makubwa, siendi popote (kutosafiri), nasubiri kuitwa au kuletewa barua ya kudaiwa kodi, kama hasara nitakuwa nimeingia. Kinachonitia wasiwasi ni jina langu, pesa si tatizo nitahangaika kuipata… tatizo ni jina langu. Wataniita fisadi, nikimalizana na serikali nitatoa tamko langu.
 

“Nimerudi Ijumaa (Novemba 21, 2015) iliyopita nilienda China na Thailand, akanipigia simu (wakala wake) usiku huo huo akaniambia alipata msiba anaelekea Kenya nikamwambia sawa, nikauliza kuhusu nyaraka zangu vipi kwa sababu kontena alishanitolea. Nikamwambia vipi….. akasema atarudi Jumatatu (Novemba 23) au Jumanne (Novemba 24), nikaona sawa. Jumatano (Novemba 25, 2015) nikampigia simu zake zote zikawa zimezimwa, Ijumaa (Novemba 27) ndiyo limekurupuka hili suala (uamuzi wa Waziri Mkuu Majaliwa na Rais Dk. Magufuli).
 

“Hapo nikapata wasiwasi huyu jamaa yangu hapatikani, nikajiuliza maswali mengi, baadaye kuna watu wakaniambia wewe upo kwenye hizo kontena zenye utata wa kodi. Inauma lakini kulipa mara ya pili ni hasara lakini kitendo kimeshafanyika. Tungeruhusiwa kulipa wenyewe (wafanyabiashara) kodi yasingetokea haya. Halafu inaingia akilini nifanye uchafu kwa kutumia jina langu nililotengeneza kwa miaka 15 kibiashara? Si ningetengeneza kampuni hewa kufanya haya? Ndiyo maana katika kampuni hizo za kontena hakuna majina makubwa ya kibiashara inawezekana wamentengeza feki,” alisema.
Ilivyokuwa kwa Bakheresa
 

Taarifa kuhusu Bakheresa zilizotolewa kwa vyombo vya habari mara baada ya sakata hilo zilieleza kwamba, kampuni ya mfanyabiashara huyo maarufu nchini, Said Salim Bakhresa (SSB) nayo ilikuwa ikichunguzwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kushiriki kukwepa kodi na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha kwa sababu ya kuhifadhi makontena hayo yenye utata wa kodi.
 


Sambamba na uchunguzi huo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekwishapiga marufuku SSB kuingiza makontena mengine kwenye bandari yake ya nchi kavu. Maagizo hayo ni kwa mujibu wa barua ya Wolfgang Salia kwa niaba ya Kamishna wa Ushuru na Forodha wa TRA, kwenda kwa Meneja wa SSB.
Barua hiyo inaieleza kampuni ya SSB kwamba, vitendo vya ukwepaji kodi vimefanywa kinyume cha Sheria ya Ushuru wa Pamoja wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004 na hivyo kuikosesha Serikali mapato. Kutokana na kuhifadhi makontena hayo, Bakheresa ameamriwa kulipa faini ya Sh bilioni 12.6, kama hatua za awali za kushughulikia kadhia hiyo.
 

Mengine ya ziada
Ingawa kusimamishwa kwa Bade kunahusishwa na sakata hilo, mtoa habari wetu amefichua tuhuma nyingine zinazoelekezwa kwa Bade, kwamba licha ya malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wateja, bosi huyo mkuu amekuwa na tabia ya kumbeba msimamizi wa masuala ya forodha bandarini, Barton Kaisi, ambaye akiwa katika nafasi hiyo, alikuwa akihusika na utoaji wa makontena bandarini.
 

Inadaiwa kwamba baada ya malalamiko ya wateja dhidi ya Kaisi, Bade alichukua hatua ya kumhamishia kitendo kingine muhimu cha Transit & Enforcement, ambacho nacho kimekuwa kikihusishwa na ufanikishaji wa nyaraka tata zinazoeleza makontena kadhaa yanapelekwa nje ya Tanzania lakini yakibaki ndani ya mipaka, na kwamba kinachofanyika, nyaraka hizo hupelekwa katika vituo vya mipaka ya Burundi na Sudan Kusini kupigwa mihuri ya kuonyesha kwamba makontena hayo yameingia kwenye nchi hizo.
 

“Kinachopelekwa kwenye boda (mipaka), hasa boda za Burundi na Sudan Kusini ni nyaraka tu na si mali, mali inagawanywa hapa hapa Tanzania. Yuko ofisa mmoja (anatajwa jina) kazi alikuwa amewekewa bajeti ya dola 100,000 kila mwezi na kampuni fulani (iliyojitangaza kufilisika hivi karibuni). Alikuwa akisaidia kampuni hiyo kutoa makontena hadi 1,000 bila ukaguzi,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.
Kwa sasa, Rais Magufuli amekwishamteua Dk. Philip Mpango kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA.
CHANZO: RAIA MWEMA

Post a Comment

Previous Post Next Post