Mwenyekiti
wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida
akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani) juu ya kazi
inayofanywa na Rais Dk. John Magufuli leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi
wa habari wakimfatilia Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) ,Ramadhan Madabida leo jijni Dar es Salaam
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WENYEVITI
wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kasi ya Rais Dk.
John Joseph Pombe Magufuli kwa kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa
kutekeleza majukumu yao, wanapongeza kwa kufanya hivyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ,Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Wawenyeviti wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema kuwa wenyeviti wanapongeza
kwa hatua hizo ambazo amezifanya Rais Dk. John Magufuli.
Amesema
watu walikuwa wanatoa huduma isiyo bora kwa wananchi hivyo kila mtu kwa
nafasi yake afanye kazi yake kwa mujibu wa sharia
Madabida
amesema kwa kasi hiyo wako tayari na maamzi yeyote ambayo anaweza
kuyatoa kwa viongozi wa CCM ambao hawakuweza kufuata utaratibu.
Aidha
amesema wananchi waunge juhudi ambazo Rais John Joseph Magufuli anafanya
katika kuweza kila mtu aweze kuwajibika ipasavyo kuwahudumia wananchi
wake.
Ameongeza
kuwa Wenyeviti wataendelea kuwa pamoja na Rais katika majumu yake ya
kuhakikisha nchi inakuwa na watendaji wanaojituma na kila nyakati ina
dhana yake


Post a Comment