DIAMOND KAVUMILIA WEEE HATIMAYE KAAMUA KUSEMA HAPIMI NG’OO DNA … ‘sipimi, mtoto awe wangu au sio wangu haiwahusu’

Msanii supastaa wa muziki wa kizazi kipya anayeipeperusha vema bendera ya TZ kimataifa, Diamond Platnumz, ameamua kuzungumzia ‘ishu’ ya uhalali wa mwanae Tiffah.

Kwa muda mrefu baadhi ya watu wamekuwa wakimpiga madogo Diamond kwa kusema Tiffah si mwanae na wakaenda mbali zaidi kwa kumtaka akapimie DNA ili kupata ukweli.

Akizungumza katika kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Jumatano usiku, Diamond akasema hana mpango wa kupima DNA.

“Mimi ndio nilipaswa kudai DNA, sio wao. Sina mpango wa kwenda kupima kwa sababu najiamini mtoto ni wangu,” alisema Diamond.

Msanii huyo akaongeza: “Hata kama mtoto si wangu au ni wangu, hiyo haiwahusu. Hebu tufanye mambo ya kuleta maendeo badala ya vitu ambavyo havina msingi.

“Unamzungumzia Tiffah ambaye anakuzidi kila kitu, Tiffah ni tajiri, anamiliki akaunti yenye pesa nyingi, sasa inakusaidia nini kumzungumzia Tiffah.

Kuna watu nimewakuta kwenye ‘game’ wamefanya muziki kwa muda mrefu lakini hawana maendeleo yoyote kwasababu ya kuendekeza vitu ambavyo havina msingi.

“Watu nimewazidi kila kitu, nimewazidi akili, nimewazidi uwezo wa kazi, sasa wanataka kutafuta kick kupitia Tiffah.”

Chanzo: Saluti5

No comments:

Post a Comment