Wastara Juma azimia kwa mshtuko kisa Bomoabomoa Dar!
MAJANGA! Bomoabomoa inayoendelea jijini Dar imemkumba msanii wa filamu, Wastara Juma aliyejikuta akizimia kwa mshtuko.
Ndugu wa karibu wa mwigizaji huyo aliliambia Ijumaa kuwa hivi karibuni Wastara aliwekewa alama ya X na maafisa wa ardhi katika nyumba zake mbili zilizopo maeneo ya Tabata-Barakuda jijini Dar kuonesha kwamba ziko kwenye eneo hatarishi.
 

STORI KAMILI
Ndugu huyo alizidi kudai kuwa, siku maafisa hao walipokuwa wanaweka alama hiyo, Wastara hakuwepo nyumbani na alipofika alishindwa kustahimili hali hiyo na kujikuta akizimia na kuzinduka mara kadhaa.“Alipozinduka aliendelea kulia siku nzima, anasikitisha kwa kweli,” alisema ndugu huyo wa karibu.
SIKU 10 ZAMPA MACHUNGU
Ndugu huyo aliendelea kusema kuwa kilichowashangaza ni kupewa siku kumi za kuondoa vitu vyao hali inayowafanya wajiulize watavipeleka wapi kwani siku ni chache.
“Unajua tumepatwa na mshtuko mkubwa kwani hata hivyo tangu tuishi hapa hatujawahi kukumbwa na mafuriko ya aina yoyote, ukiuliza ni kwa nini wameamua kufanya hivyo unaambiwa sehemu hatarishi, kiukweli hatuna la kufanya tumechanganyikiwa,” alisema ndugu huyo.
IJUMAA MZIGONI
Baada ya ndugu kuelezea tukio hilo, Ijumaa lilifunga safari hadi Tabata-Barakuda, zilipo nyumba zake hizo na kuzungumza naye.
ASHINDWA KUNYANYUKA
Waandishi walipotaka kuonana na Wastara kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na suala hilo alishindwa kunyanyuka kitandani hivyo kulazimika kumfuata chumbani.
AFUNGUKA, AANGUA KILIO
“Sijui nina nini jamani, serikali ingeniangalia ni juzi tu nimemaliza nyumba yangu, hapa nilipo natafuta hela nyingi tu niende kwenye matibabu ya mguu wangu sijapata linakuja hili ha! (analiaaa).
ATESWA NA FAMILIA
“Naifikiria sana familia yangu ni kubwa sijui nitaipeleka wapi na shida niliyonayo nimechanganyikiwa, namuomba Mungu kiukweli,” alisema

No comments:

Post a Comment