Abdu Kiba amesema wakati anafanya video yake mpya ya wimbo Bayoyo,
alikutana na changamoto za hapa na pale moja ambayo iliyomsikitisha
zaidi ni baada ya model aliyekuwa anatakiwa kufanya kutotokea na
kutopokea simu zake katika hatua za mwisho.

Hiyo ilimfanya kutafuta mbadala wa haraka.
“Unajua mrembo ambaye nilitakiwa kufanya naye video ni yule ambaye
alifanya video ya Raymond ambaye nilipanga naye kila kitu hadi tarehe ya
siku ya kusafiri kwenda kufanya video lakini baadaye simu huyo mrembo
akawa hapokei na baadaye akazima simu,” Abdu alikiambia kipindi cha
Clouds E.

“Hiyo kwangu ilikuwa changamoto ambayo ilinitatiza sana na hiyo yote
ni kwa sababu ya mambo ya team hizi ndio maana hakuweza kufanya video
yangu ila siku ya siku ndio akapatikana model yule mwingine video
ikafanyika.”
Post a Comment