Baadhi ya wanaharakati anuai wakiwa na maua walipomtembelea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka kumfariji jana.
Baadhi ya wanaharakati wakiwa na nyoso za hudhuni baada ya kilio cha baba wa Dk. Ulimboka jana MOI.
Baba
wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda (katikati)
akipokea faraja kwa niaba ya mwanaye toka kwa wanaharakati (hawapo
pichani).
Baba
wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda (kushoto)
akipokea kadi yenye ujumbe toka kwa wanaharakati walipomtembelea jana,
anayetoa kadi hiyo (kulia) ni Mkurugenzi wa TGNP, Usu Mallya.
Baba
wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda (kushoto)
akipokea ua kutoka kwa mwakilishi wa wanaharakati anuai waliomtembelea
kumfariji.
BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda.
Baba wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda akilia na kufarijiwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha
Habari na Mawasiliano, Lilian Liundi walipomtembelea Dk. Ulimboka
kumfariji jana.
Mwakilishi wa wanaharakati, Markos Albania (katikati) akizungumza na wanahabari baada ya kumtembelea Dk. Steven Ulimboka.
Mzee Steven Mwaitenda (katikati) akifarijiwa na kurejeshwa wodini baada ya kulia.
Usu Mallya akilia baada ya kushuhudia mzee Steven Mwaitenda akibubujikwa na machozi mbele yao.
Na Joachim Mushi, Thehabari.com
Baba
wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda amejikuta
akiangua kilio kwa uchungu mbele ya wanaharakati ambao walimtembelea
mwanae, Dk. Steven Ulimboka kumpa pole kufuatia tukio la kutekwa na
kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.
Hali
hiyo ilitokea jana jioni katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili
(MOI), ambapo wanaharakati kutoka taasisi na asasi mbalimbali za utetezi
wa haki za binadamu walifika kwa lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka
kufuatia kitendo kilichomfika.
Mzee
Mwaitenda alijikuta akibubujikwa na machozi na kushindwa kuendelea
kuzungumza alipokuwa akitoa shukrani kwa wanaharakati hao, kwa niaba ya
mwanaye ambaye wanaharakati hao walishindwa kumuona wote kutokana na
hali yake ilivyo sasa.
“Niseme
wazi nimefarijika sana kwa ujio wenu kumwona mwanangu dhidi ya mambo ya
kikatili aliyofanyiwa akitetea haki za wengine…,” alisema mzee
Mwaitenda kabla ya kushindwa kuendelea na kuangua kilio mbele ya
wanaharakati.
Baada
ya tukio hilo baadhi ya wanaharakati walimshika wakishirikiana na
wanafamilia ya mzee Mwaitenda na kumbebeleza kisha kumtoa mbele ya
mkusanyiko huo wa wanaharakati na kumrudisha wodini huku wakimfariji.
Wakizungumza
mara baada ya tukio hilo wanaharakati wameelezea kusikitishwa na
vitendo vinavyoendelea MOI eneo ambalo amelazwa kiongozi huyo wa
madaktari ambavyo vimeendelea kutishia usalama wa Dk. Ulimboka.
Akifafanua
zaidi mwakilishi wa wanaharakati hao, Markos Albania alisema taarifa
walizozipata usiku wa juzi kuna wagonjwa ‘feki’ ambao walijitokeza MOI
huku wakitaka kulazwa wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) alipolazwa Dk.
Ulimboka lakini baadaye waligoma kuingizwa wodini.
“Wapo
wagonjwa ambao waliletwa na kutaka kupelekwa ICU moja kwa moja…kuna
watu wanakuja usiku wa manane wakitaka kumtembelea Dk. Ulimboka…matendo
yanayoendelea kutokea ukilinganisha na kauli za Serikali zilizotolewa
bungeni yanatishia usalama na uhai wa mgonjwa,” alisema Albania.
Aidha
amesema kitendo cha vyombo vya usalama kuendelea kumuhoji Dk. Ulimboka
akiwa hoi hospitalini si vya kiungwana kwani tayari muhusika amewataja
hadi kwa majina watu ambao anawashuku lakini hadi sasa hakuna
aliyechukuliwa hatua yoyote.
Pamoja
na hayo wanaharakati hao wameitaka Serikali kuunda tume huru
mchanganyiko na raia ambayo itachunguza kiundani suala hilo, kwani
hawana imani na Jeshi la Polisi ambalo limedai kuunda timu ambayo
inachunguza kwa kina suala hilo.
Dk.
Ulimboka ambaye ni kiongozi wa madaktari ambao wanaendelea na mgomo wa
nchi nzima kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao alitekwa juzi na
watu wasiojulikana na kupigwa na kuteswa kikatili kabla ya kutelekezwa
katika msitu wa Mabwepande.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
Post a Comment