Miss
Utalii Tanzania, tofauti na mashndano mengine ya urembo, ni zaidi ya
shindano la urembo, kwani linalenga katika kutangaza na kuhamasisha
Utalii,Utamaduni, Mianya ya Uwekezaji,Elimu,Afya ya Jamii,Utalii wa
ndani,Utalii wa kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikitano
Kitaifa na kimataifa. Shindano hili pia linahamasisha vita dhidi ya
Umasikini,Iharibifu wa mazingira,uwindaji haramu,Uvuvi
Haramu,Ujinga,Maradhi, Tamaduni kongwe na Potofu.
Miss
Utalii Tanzania pamoja na uchanga wake, tangu kuanzishwa kwake mwaka
2005, ni shindano lenye mafanikio makubwa kuliko shindano jingine lolote
nchini kitaifa na kimataifa kwani pamoja na kuipa heshima Tanzania ya
kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la Miss Tourism World 2006, shindano
hili ndilo lililo andika historia ya Tanzania kutwaa taji la kwanza la
Dunia kabla na baada ya uhuru, pale tulipo twaa taji la Miss Tourism
World 2006, pia shindano hili ndilo pekee nchini linashikilia rekodi ya
kutwaa mataji ya dunia katika kila shindano tulilo shiriki,tumetwaa
mataji 6 ya dunia tangu 2005.
Kutokana
na mafanikio haya , Tumepewa heshima ya kuaandaa shindano la Dunia la
Miss Umoja wa Mataifa mwaka 2013 hapa Tanzania. Ni shindano pekee nchini
ambalo washiriki wake hawavai mavazi ya kuogelea, bali mavazi ya
heshima yasiyo mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yaliyo buniwa na
kushonwa kwa malighafi za tanzania tu.
Link yetu ni : http://misstourismorganisation.blogspot.com/
Facebook Page: https://www.facebook.com/MissUtaliiTanzania
E-Mail: missutaliitanzania@gmail.com
Asanteni sana.
Miss Tourism Organisation Tanzania.
Post a Comment