VYAMA vya siasa vya upinzani vya Chadema na CUF vimesema havina imani
na tume iliyoundwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuchunguza tukio
la kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari
Tanzania, Dk Steven Ulimboka.
Badala yake vimetaka iundwe tume huru itakayohusisha vyombo vya dola, madaktari na asasi zisizo za kiserikali.
Taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti na vyama hivyo viwili, zilisema vyote vinaamini kuwa kwenye tukio hilo la kinyama lina mkono wa Serikali.

Sekretarieti
ya Chadema ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson
Kigaila, jana ilitishia kuunganisha nguvu ya umma katika kuibana
Serikali kama tume hiyo haitakuwa tayari kuunda tume huru.Akizungumza na
waandishi wa habari, Kigaila waliilaumu Serikali kwa kitendo chake cha
kushindwa kutekeleza madai ya madaktari, wakati ikiruhusu fedha yingi
kupotea kwa njia za uzembe na ufisadi.
Alisema historia inaonyesha kuwa matukio mengi yaliyochunguzwa na polisi, matokeo yake hayajawekwa hadharani.
Mkurugenzi huyo alisema matukio hayo ni mauaji ya watu wawili yaliyotokea katika chaguzi ndogo za Igunga na Arumeru mashariki.
Hali kadhalika, tukio la kumwagiwa tindikali kwa mwandishi wa habari Seid Kubenea.Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Haki za Binadamuna wa CUF, Abdul Kambaya ilisema Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kwa kuunda tume huru bila kuhusisha Jeshi la Polisi ili uchunguzi wa kina tukio hilo.

Post a Comment