Najenga Simba ya Ligi Kuu - Cirkovic

KOCHA wa timu ya Simba Mserbia, Milovan Cirkovic, amesema anataraji kikosi chake kitafanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu kwani kwa sasa anaelekeza nguvu zote kwenye ligi msimu ujao.

Akizungumza jijini juzi kwenye Viwanja vya Sigara Chang'ombe ambako timu hiyo inapiga 'tizi', alisema kuwa mkazo wake zaidi ni kwenye ligi kwa kuwa Kombe la Kagame ni mashindano ya wiki mbili tu.

"Nitaingia kwenye Kagame kwa lengo la kusaka ubingwa, lakini nguvu nyingi nitazielekeza kwenye Ligi Kuu ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kimataifa.

"Unajua nikifanya vibaya kwenye ligi siwezi kupata nafasi ya kushiriki  kwenye Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho Afrika ndiyo maana naelekeza nguvu zangu kwenye ligi zaidi."

Kuhusiana na hali ya mazoezi inavyoendelea Milovan alisema wachezaji wake hadi sasa wanaonekana kuelewana kiasi kwamba ana matumaini ya kufanya vizuri katika michezo iliyo mbele yao.

Alisema beki mpya wa klabu hiyo Masombo Lino, kutoka DC Motema Pembe kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anaimudu vema nafasi yake hiyo na kufanya wasiwasi kuhusu Kelvin Yondan umtoke.

"Wachezaji wapo vizuri nimependa wanavyofanya mazoezi kwa kuelewana na nilikuwa nina wasiwasi na nafasi ya Kelvin Yondan ambaye hayupo lakini huyu kutoka Motema Pembe ameiziba na anamudu vema kuzuia na kusaidia mashambulizi pia" alisema.
xxx
Katika hatua nyingine kocha huyo atawakosa nyota wake beki  Kelvin Yondani na  kipa Ally Mustapha 'Barthez' waliojiunga na Yanga, winga Salum Machaku alipelekwa Mtibwa Sugar.

Beki raia wa Uganda, Derick Walulya, mshambuliaji Jamhuri ya Afrika Kati, Gervais Kago wameachwa.

Beki mwingine ambaye ametangazwa kuachwa ni Juma Jabu na Salum Kanoni ambaye hata hivyo, mkataba wake umebakisha siku mbili kumalizika.

Wachezaji ambao klabu hiyo inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka,  Haruna Shamte na Shija Mkina. Mkina bado anacheza kwa mkopo Kagera Sugar.

Post a Comment

Previous Post Next Post