KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovick jana alianza rasmi kuinoa timu
hiyo inayojiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, huku akisifu kiwango
kizuri cha wachezaji wapya waliosajiliwa hivi karibuni.
Cirkovick aliwasili nchini mwanzoni mwa wiki hii akitoka nchini Serbia ambako alikwenda kwa mapumziko baada ya kumalizika Ligi Kuu Bara.
Cirkovick aliwasili nchini mwanzoni mwa wiki hii akitoka nchini Serbia ambako alikwenda kwa mapumziko baada ya kumalizika Ligi Kuu Bara.
Akizungumza
na Mwananchi jana, Cirkovick alisema kuwa amekuja na mbinu mpya ambazo
baadhi ameanza kuzitoa kwenye mazoezi ya jan Viwanja vya TCC Chang'ombe.
"Nina matuini makubwa vijana wangu watazielewa haraka mbinu hizi kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kagame," alisema kocha huyo.
"Nina matuini makubwa vijana wangu watazielewa haraka mbinu hizi kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kagame," alisema kocha huyo.
"Najiridhisha
na uwezo wa kuelewa wa wachezaji wangu, sina shaka kwamba kabla ya
kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame watakuwa tayari wameshaelewa,"
alisema Cirkovick.
Kuhusu wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, Cirkovick aliwasifu wachezaji hao na kusema watakuwa na mchango mkubwa msim huu.
Kuhusu wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, Cirkovick aliwasifu wachezaji hao na kusema watakuwa na mchango mkubwa msim huu.
"Kwa sasa tunajipanga kuhakikisha tunajenga mfumo mmoja utakaoeleweka haraka kati ya wachezaji wa zamani na wale wapya."
Alisema
pamoja na kutoshiriki kwenye zoezi la usajili, nameridhika wale
waliofanya kazi hiyo kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na kujituma pia.
Katika
hatua nyingine, uongozi wa Simba utahakikisha timu hiyo inakuwa katika
mazingira mazuri yatakayowawezesha wachezaji kufanya mazoezi vizuri.
Ofisa
habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kwamwaga alisema baada ya ziara ya Kanda
ya Ziwa, pia wana mpango wa kuiandalia timu mechi kadhaa za kirafiki
Post a Comment