Cirkovick asifu usajili Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovick jana alianza rasmi kuinoa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, huku akisifu kiwango kizuri cha wachezaji wapya waliosajiliwa hivi karibuni.
Cirkovick aliwasili nchini mwanzoni mwa wiki hii akitoka nchini Serbia ambako alikwenda kwa mapumziko baada ya kumalizika Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Mwananchi jana, Cirkovick alisema kuwa amekuja na mbinu mpya ambazo baadhi ameanza kuzitoa kwenye mazoezi ya jan Viwanja vya TCC Chang'ombe.
"Nina matuini makubwa vijana wangu watazielewa haraka mbinu hizi kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kagame," alisema kocha huyo.
"Najiridhisha na uwezo wa kuelewa wa wachezaji wangu, sina shaka kwamba kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame watakuwa tayari wameshaelewa," alisema Cirkovick.
Kuhusu wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, Cirkovick aliwasifu wachezaji hao na kusema watakuwa na mchango mkubwa msim huu.
"Kwa sasa tunajipanga kuhakikisha tunajenga mfumo mmoja utakaoeleweka haraka kati ya wachezaji wa zamani na wale wapya."
Alisema pamoja na kutoshiriki kwenye zoezi la usajili, nameridhika wale waliofanya kazi hiyo kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na kujituma pia.
Katika hatua nyingine, uongozi wa Simba utahakikisha timu hiyo inakuwa katika mazingira mazuri yatakayowawezesha wachezaji kufanya mazoezi vizuri.
Ofisa habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kwamwaga alisema baada ya ziara ya Kanda ya Ziwa, pia wana mpango wa kuiandalia timu mechi kadhaa za kirafiki

Post a Comment

أحدث أقدم