DROGBA AHAMIA CHINA

DROGBA AHAMIA CHINA

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba (Pichani) ameingia mkataba na Klabu ya mpira wa miguu ya China ijulikanayo kama Shanghai Shenhua FC ya China, imefahamika kuwa Dgroga kasaini Mkataba wa miaka miwili na nusu na atajiunga rasmi na timu hiyo mwezi July  mwaka huu,  mkataba huo kati ya Drogba na Klabu hiyo unategemea kuisha  mwishoni mwa mwaka 2014.

Kupitia Website yake Drogba alifunguka na kusema " Nimepokea mialiko mingi kwa wiki za hivi karibuni ila nimefikiri  kuwa Shanghai Shenhua FC ni timu nzuri ya kujiunga nayo kwa sasa, Ninatarajia changamoto nyingi mpya ikiwemo  kujifunza mila na desturi mpya, pia nina shauku  na maendeleo mapya  katika mpira wa China"

Inasemekana Drogba alitembelea nchi ya China mwaka jana na mapokeo yao yalikuwa mazuri na kugundua kuwa na washabiki wengi.  Drogba pia alisisitiza kusaidia kukuza soka la China na kuhakikisha anatengeneza mahusiano mazuri kati ya China na Afrika

Imefahamika kuwa Shanghai Shenhua FC inammiliki mchazaji mwingine wa zamani wa Chelsea anayejulikana na Nicolas Anelka.

Chanzo  Habari 

Post a Comment

أحدث أقدم