HIZI NDIZO PICHA ZA MAJERUHI WA AJALI YA TEGETA LEO

HIZI NDIZO PICHA ZA MAJERUHI WA AJALI YA TEGETA LEO






Majeruhi aliyeumia sehemu za kichwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mwananyamala.




Majeruhi katika ajali ya leo huko Tegeta akipatiwa huduma na wauguzi wa hospitali ya Mwananyamala.



Frank Mmari (34) mkazi wa Bunju 'A' akiwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kupata ajali iliyotokea Tegeta leo.



Lewina Selekwa akipatiwa huduma ya maji ndani ya hospitali ya Mwananyamala.

Lewina Selekwa akiwa na jamaa zake.
 Pichani juu ni majeruhi wa ajali 
iliyotokea leo Tegeta Kibaoni njia panda ya Wazo Hill jijini Dar es
Salaam baada ya lori moja kuligonga basi la abiria kwa nyuma baada ya
dereva wake kushindwa kuliongoza, hivyo kuliparamia basi. Kwa mujibu wa
taarifa ya Mganga Mkuu Hospitali ya Mwananyamala, Dk Sophinias Ngonyani
watu waliopata ajali katika tukio hilo ni 11, kati ya hao 2 wamefariki
dunia na mmoja ametambuliwa na ndugu zake kwa jina la Halima Salim
Msulwa (40) na mwingine ni mwanaume ambaye mpaka sasa hajajulikana jina
lake. Wengine 3 wamevunjika mikono na kupelekwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu zaidi, wakati waliosalia wamepata matibabu na
kuruhusiwa. (PICHA ZOTE NA MAKONGORO OGING'/GPL)

Post a Comment

أحدث أقدم