Melfu ya waandamanaji wamefurika katika medani ya
Tahrir mjini Cairo, Misri kulaani watawala wa kijeshi kwa kujiongezea
madaraka makubwa. Wiki iliyopita
Waandamanaji Misri
watawala wa kijeshi walifuta
bunge na
kujilimbikizia mamlaka ya kutunga sheria.
Raia wa Misri wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa
Urais ambao mgombea wa mrengo wa Muslim Brotherhood Mohammed Mursi
anataka yatolewe mara moja.
Wanajeshi wametetea hatua yao wakisema inasaidia
kukabiliana na tisho lolote la usalama. Katika taarifa kupitia runinga
ya taifa, Baraza la utawala wa Kijeshi limelaumu mgawanyiko wa kisiasa
ulioko nchini kwa kusababisha ucheleweshwaji wa matokeo hayo.
Baraza hilo halijataja lolote kuhusu mgombea wa
chama cha Freedom and Justice ambacho hapo Jumanne kilisema bw Mursi
alikua ameshinda uchaguzi kwa asili mia 51.7.
Mpinzani wake Ahmed Shafiq ambaye aliwahi kua
Waziri Mkuu ametangaza pia kushinda.Makundi yanayotetea sera isiyofuata
dini na wanaharakati wa kiisilamu wameitikia maandamano yaliyoitishwa na
Muslim Brotherhood baada ya sala ya Ijumaa.
Viongozi wa kidini walioongoza maombi katika
medani ya Tahrir walisema Mohammed Mursi ndiye mshindi katika raundi ya
pili ya uchaguzi wa pili.Akihutubia waandishi wa habari Mursi alisema
atakubali matokeo ikiwa shughuli nzima itafanyika kwa njia ya uwazi.
Aliongeza endapo atatangazwa Rais atahakikisha Misri inapata Waziri Mkuu anayeungwa na pande zote.
Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights
Watch limesema mzozo wa sasa unavunja matumaini ya kuyakabidhi madaraka
kwa raia nchini Misri na hivyo kuyumbisha mchakato wa demokrasia.
Chanzo:- BBC Swahili
Chanzo:- BBC Swahili
Post a Comment