Maelfu waandamana Misri dhidi ya Jeshi

Melfu ya waandamanaji wamefurika katika medani ya Tahrir mjini Cairo, Misri kulaani watawala wa kijeshi kwa kujiongezea madaraka makubwa. Wiki iliyopita 

Waandamanaji Misri 
watawala wa kijeshi walifuta 
bunge na kujilimbikizia mamlaka ya kutunga sheria.
Raia wa Misri wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa Urais ambao mgombea wa mrengo wa Muslim Brotherhood Mohammed Mursi anataka yatolewe mara moja.
Wanajeshi wametetea hatua yao wakisema inasaidia kukabiliana na tisho lolote la usalama. Katika taarifa kupitia runinga ya taifa, Baraza la utawala wa Kijeshi limelaumu mgawanyiko wa kisiasa ulioko nchini kwa kusababisha ucheleweshwaji wa matokeo hayo.
Baraza hilo halijataja lolote kuhusu mgombea wa chama cha Freedom and Justice ambacho hapo Jumanne kilisema bw Mursi alikua ameshinda uchaguzi kwa asili mia 51.7.
Mpinzani wake Ahmed Shafiq ambaye aliwahi kua Waziri Mkuu ametangaza pia kushinda.Makundi yanayotetea sera isiyofuata dini na wanaharakati wa kiisilamu wameitikia maandamano yaliyoitishwa na Muslim Brotherhood baada ya sala ya Ijumaa.
Viongozi wa kidini walioongoza maombi katika medani ya Tahrir walisema Mohammed Mursi ndiye mshindi katika raundi ya pili ya uchaguzi wa pili.Akihutubia waandishi wa habari Mursi alisema atakubali matokeo ikiwa shughuli nzima itafanyika kwa njia ya uwazi.
Aliongeza endapo atatangazwa Rais atahakikisha Misri inapata Waziri Mkuu anayeungwa na pande zote.
Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema mzozo wa sasa unavunja matumaini ya kuyakabidhi madaraka kwa raia nchini Misri na hivyo kuyumbisha mchakato wa demokrasia.
Chanzo:- BBC Swahili

Post a Comment

أحدث أقدم