MAJINA YA WAKURUGENZI 8 WALIOFUTWA KAZI, 11 WALIOPEWA ONYO,14 WAPYA NA 22 WALIOHAMISHWA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewavua madaraka wakurugenzi watendaji wanane wa halmashauri pamoja na kuwapumzisha kazi wakurugenzi watatu, huku wakurugenzi 11 wakipewa onyo.

Hatua hiyo imekuja miezi michache baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), Ludovick Utouh kugundua ubadhirifu mkubwa katika Serikali za Mitaa nchini ambayo ipo katika taarifa yake.

Katika Mkutano wa Saba wa Bunge uliofanyika Aprili mwaka huu, CAG aliwasilisha taarifa zake ambazo pamoja na mambo mengine, zilionesha ubadhirifu mkubwa katika Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa, na wabunge kuja juu wakitaka wahusika waadhibiwe.

Mbali na hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amewateua wakurugenzi wapya 14 na kuwahamisha vituo vya kazi wakurugenzi 22 ili kuimarisha utendaji kazi katika Halmashauri. Ghasia alitangaza uamuzi huo wa Serikali jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, akiwa na Naibu Mawaziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri (Tamisemi) na Kassim Majaliwa (TAMISEMI – Elimu).

Alisema maamuzi hayo yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12, lengo ni kuboresha utendaji kazi katika Serikali za Mitaa nchini.

Alisema wakurugenzi waliovuliwa madaraka, waliopewa onyo na waliopumzishwa kazi walionekana kutotimiza wajibu wao hivyo wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Wakurugenzi waliovuliwa madaraka na vituo vyao vya kazi ambapo makosa yalifanyika kuwa ni:

1.       Consolata Kamuhabwa, (Halmashuri ya Wilaya ya Karagwe)

2.       Ephraim Kalimalwendo (Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa)

3.       Elly Mlaki (Halmashauri ya Wilaya ya Babati)

4.       Eustach Temu (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza)

5.       Jacob Kayange (Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro)

6.       Hamida Kikwega (Halmashauri ya Wilaya ya Chato)

7.       Majuto Mbuguyu (Halmashauri ya Jiji la Tanga)

8.       Raphael Mbunda (Halmashauri ya Manispaa ya Arusha)

Wakurugenzi waliopumzishwa kazi ni:

1.       Xavier Tiweselekwa (Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi),

2.       Erika Mussica aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Sengerema

3.       Theonas Nyamhanga,aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu

Wakurugenzi waliopewa onyo na vituo vyao vya kazi ni:

1.       Judetatheus Mboya (Halmashauri ya Wilaya ya Newala)

2.       Lameck Masembejo (Halmashauri ya Wilaya ya Masasi)

3.       Abdallah Njovu (Halmashauri ya Wilaya Tandahimba)

4.       Jane Mutagurwa (Halmashauri ya Wilaya Shinyanga)

5.       Silvia Siriwa (Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga)

6.       Lewis Kalinjuna (Halmashauri ya Kigoma)

7.   Kelvin Makonda (Halmashauri ya Bukombe

8.   Alfred Luanda (Halmashuri ya Ulanga)

9.   Fanuel Senge (Halmashauri ya Tabora)

10.   Beatrice Msomisi (Halmashauri ya Bahi)

11.   Maurice Sapanjo (Halmashauri ya Wilaya ya Chunya)

Wakuregenzi wapya walioteuliwa ni:-

1.       Jenifer Omoro (Halmashauri ya Mji wa Kibaha)

2.       Fidellica Myovela (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma)

3.       Hadija Makuwani (Manispaa ya Tabora)

4.       Ibrahimu Matovu (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza)

5.       Idd Mshili (Halmashajuri ya Mtwara)

6.       Julias Madiga (Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro)

7.       Kiyungi Mohamed Kiyungi (Halmashauri ya Shinyanga)

8.       Lucas Mweri (Mtendaji wa Wilaya ya Namyumbu)

9.       Miriam Mmbaga (Halmashauiri ya Wilaya ya Kigoma)

10.   Mwamvua Mrindoko (Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea)

11.   Pendo Malembeja (Halmashauri ya Wilaya Kwimba)

12.   Pundenciana Kisaka (Halmashauri ya Wilaya Ulanga)

13.   Ruben Mfune (Halmashauri ya Wilaya Ruangwa)

14.   Tatu Selemani (Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha)

Ghasia alisema uteuzi huo wa wakurugenzi umeanza tangu Aprili 24, 2012.

Wakurugenzi waliohamishwa na vituo vyao vya kazi ni:

1.       Eizabeth Kitundu ambaye anatoka Maswa kwenda Misenyi

2.       Afred Luanda anatoka Ulanga kwenda Kigoma Ujiji

3.       Robert Kitimbo anatoka Mpwapwa kwenda Manispaa ya Dodoma

4.       Shaaban Ntarambe anatoka Kwimba kwenda Chato

5.       Francis Namaumbo anatokea Masasi kahamishiwa Mafia

6.       Hilda Lauwo anatoka Ludewa anahamishiwa Maswa

7.       Fanuel Senge anatoka Manispaa ya Tabora anahamishiwa Mpwapwa

8.       Upendo Sanga natoka Meatu anahamishiwa Mbeya

9.       Isaya Mngurumi anatoka Kisarawe anahamishiwa Meatu

10.   Lewis Kalinjuna anatokea Kigoma Ujiji anahamishiwa Korogwe

11.   Dominic Kweka anatoka Kigoma anahamishiwa Babati

12.   Lameck Masembejo ambaye anahamishiwa Kilosa akitokea Korogwe

13.   Azimina Mbilinyi anatokea Kibaha anakwenda Kilombero

14.   Bosco Ndunguru anatokea Kilolo anakwenda Kilolo

15.   Karaine Ole Kuney anatokea Musoma anakwenda Ngorongoro

16.   Mohamed Ngwalima anatokea Mtwara kwenda Kilolo

17.   Gladys Dyamvunye anatokea Nanyumbu kwenda Masasi

18.   Eden Munis kutoka Morogoro kwenda Ludewa

19.   Christina Midelo kutoka Korogwe kwenda Iramba

20.   Anna Mwahalende kutoka Moshi kwenda Korogwe

21.   Mathias Mwangu kutoka Ngara kwenda Singida

22.   Yona Maki kutoka Manispaa ya Singida kwenda Kisarawe

Alisema baadhi ya wakurugenzi watendaji waliovuliwa madaraka na wale waliopumzishwa kazi walionekana kuhusika na ubadhirifu wa fedha na wengine walionekana kutomudu madaraka ya ukurugenzi na hivyo kupewa majukumu mengine.

Alisema kwa wale waliohusika na ubadhirifu, baadhi yao wamefikishwa mahakamani na wengine uchunguzi bado unaendelea wakibainika kuhusika watafikishwa mahakamani.

Aliwataja waliofikishwa mahakamani hadi sasa kuwa ni Harold Senyagwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kyela na Rhoda Nsemwa, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo.

Ghasia aliwataka wakurugenzi wote, ikiwemo wale wapya, waliohamishwa vituo na waliopewa onyo kuwajibika ili thamani ya fedha ionekane kutokana na huduma zinazotolewa kwa wananchi.

---
Taarifa hii imepatikana via magazeti ya HabariLeo, MTANZANIA na Mwananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post