Serikali ya Uganda inapanga
kupiga marufuku mashirika 38 yasio ya kiserikali kwa kigezo kwamba
zinachochea mapenzi ya jinsia moja.
Lakini waziri huyo hakuyataja mashirika hayo ambayo amepanga kuyaharamisha.
Nchini Uganda mapenzi ya jinsia moja ni hatia na kwa wakati huu hoja ya inayopendekeza watakaopatikana wakishiriki katika mapenzi ya aina hiyo wafungwe jela maisha ingali bungeni.
Uganda ni nchi ambayo inashikilia maadili ya kiafrika na wengi wanasema kuwa mapenzi ya jinsia moja inakwenda kinyume na dini na maadili ya kiafrika.
Nchini humo watu wanaoshiriki mapenzi ya aina hiyo wamekuwa wakishambuliwa, wakifutwa kazi huku wengine wakitengwa na jamii.
Ni kutokana na hali hiyo ambapo hivi karibuni mashirika ya kutetea haki za watu wanaofanya mapenzi ya yamekuwa yakiubuniwa .
Ni makundi kama hayo ndio waziri Lokodo amesema anataka yapigwe marufuku.
Post a Comment