Shirika
la ndege la Precision Air la jijini Dar es Salaam, Tanzania leo
limezindua safari yake mpya ya kwenda Lusaka, Zambia kupitia Lubumbash
nchini Congo DRC.
Kuanza
kwa safari hiyo mpya hii leo kumepokelewa kwa shangwe na
wafanyabiashara wa nchi za Zambia na Congo na wale wa Tanzania maana
sasa hawatalazimika kupitia Nairobi wala Johannesburg Afrika Kusini
wakitaka kwenda Lusaka ama Dar es Salaam.
Kwakutumia
ndege PW 704 hivi sasa safari ya Dar es Salaam hadi Lusaka itachukua
saa 2 na robo badala ya zaidi ya saa kumi ambazo abiria alikuwa
akizitumia awali kwa kupitia Nairobi.
Safari hiyo mpya ya Precision Air imezinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Precision Air, Alfonse Kioko akiteremka katika ndege na
Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kangoma baada ya kuwasili
katika uwanja wa Kimataifa wa Kenth Kaunda mjini Lusaka Zambia leo.
Kioko akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Zambia
Bendera zikiashiria ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania
MD wa Precision Air Alfonse Kioko akiongozana na Naibu Waziri wa Uchukuzi Zambia
Abiria na watumishi wa Precision Air wakiwa Lusaka
Abiria
wa kwanza wa safari ya ndege PW 704 ya Shirika la Ndege la Precision
Air wakipokelewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Keneth Kaunda mjini
Lusaka leo baada ya kuwasili salama wakitokea jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakijadili jambo. Kushoto ni Balozi wa tanzania nchini Zambia.
Cabin Crew hiyo nayo
Marubani waliofanikisha ndege hiyo PW 704 kufika uwanja wa Keneth Kaunda mjini Lusaka zambia wakilamba picha.
Post a Comment