Sir Andy Chande Mtanzania wa Kwanza kukiri wazi kuwa ni Mwanachama wa Freemason
~
“Nilipoanza kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambua
kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya
kujitenga na dunia.”
~ Asema “Nina hati “takatifu” ya kuhani mkuu freemason”
~ kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ilianzishwa Zanzibar mwaka 1904
Sir
Andy Chande ni mtanzania wa kwanza kukiri kuwa ni mwanachama wa kundi
la Freemasons, Chande tofauti na kuwa member wa kundi hilo pia
anakiri kuwa ameshika nyadhifa nyingi ndani ya kundi hili ikiwa ni
pamoja na kutunukiwa hati takatifu ya Kuhani Mkuu. Katika maelezo yake
pia ametaja asasi zilizofadhiliwa na kundi hilo lililoenea duniani
kote.
Maisha yake kama mwanachama wa kundi hilo ameyaweka katika kkitabu chake Katika alichokiita SHUJAA KATIKA AFRIKA, safari kutoka Bukene.
Mzee
Chande ni Mtanzania aliyewahi kushika nyazifa mbali mbali katika
utumishi wa umma katika Serikali ya Tanzania na kujizolea sifa kadhaa
ikiwa ni pamoja na Heshima ya “Sir” aliyopewa na Malkia wa Uingereza.
Katika
kitabu hicho ameeleza kwa kina jinsi alivyoingia katika chama hicho
Oktoba 25, mwaka 1954, akianzia na kambi inayoitwa Jaha iliyomaanisha
kundi la watu wa daraja la nne.
Kati
ya mwaka 1967 na 2003 Sir Andy Chande amekuwa mwenyekiti wa Tanzania
Tourist Corporation, Tanganyika Standard Newspapers Ltd, East African
Harbours Corporation, East African Railways Corporation and Cargo
Handling Company of East Africa ltd.Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya
Afrika mashariki Sir Chande alikuwa mwenyekiti wa Air Tanzania
Corporation na baadaye akafanya kazi kama Mwenyekiti Mamlaka ya Bandari
Tanzania na pia Mwenyekiti wa read more --->
Tanzania Railways Corporation.
Tanzania Railways Corporation.
Katika
Ukurasa wa 168 wa kitabu hiki kilichozinduliwa kwa heshima na
viongozi wa wakuu wa serikali ya Tanzania, Sir Chande anasema:
Jengo la Freemasons lililoko
maeneo ya Posta jijini Dar es salaam
|
“Kuwa
mwanachama wa Freemason maana yake ni mtu kujitolea kuingia katika
safari ndefu isiyo na mwisho ya kujifunza na kuchunguza. Kwa muda wa
miaka 50 iliyopita mafunzo yangu ndani ya Freemason yaniwezesha kupata
shahada nyingi za ngazi na umuhimu unaozidiana, ukiacha ukuu wa Wilaya
nzima ya Afrika Mashariki, yaani Kenya Sheli Sheli, Tanzania na
Uganda, kwa miaka 19. Nikitaja nafasi chache tu nilizoshika, nimekuwa
msimamizi wa kwanza mdogo kasha mkubwa wa kambi kuu ya viongozi wa
Freemasons wa Uingereza na Wiles.
Mara
ya kwanza kabisa nafasi hiyo kushikwa na mtu asiye mkazi wa
Uingereza. Nimepewa heshima ya kuwa mstahiki kamanda wa kambi ya
Donyo sabuki ya royal Ark Mariner na nimeshika uongozi wa kambi hiyo
toka mwaka 1990.
Mimi ni msimamizi mkuu wa Afrika mashariki wa kikosi kikuu cha Freemason cha Royal Ark cha Uingereza,
nikiwa nimeshika nafasi hiyo tangu mwaka 1980, na ofisi ya wilaya
tangu mwaka 1972. Mwaka 2000 nikawa Naibu Mshika upanga mkuu wa kikosi
kikuu, na bado mimi ni mkufunzi mkuu wa heshma katika kikosi kikuu
cha Uskochi.
Mwaka
1987 nilipata shahada ya Mtakatifu Lawrence, shahidi; Shada ya shujaa
wa Constantinople hati takatifu ya Kuhani Mkuu na Wawekezaji wakuu wa
Suleiman; nikapata vilevile hati muhimu ya ushujaa ya msalaba
mwekundu wa babeli mwaka 1988, nikaingia katika halmashauri ya
wasimazimi wakuu namba 1, walioteuliwa na waliokuwa hodari mno nchini
Uingereza na Wales, na nikapewa shahada ya msimamizi bora kuliko
wengine wote. Mwaka uliofuata nikaingia kama mwanafunzi wa mkataba katika jamii ya waabudu wa Freemasons, tawi la Row Assemblege”.
Katika
maelezo ya Sir Chande hapo juu kama yaliyonukuliwa katika kitabu
chake hicho chenye kuheshimiwa sana nchini napengine hata duniani, yapo
mambo mawili yenye kuhitaji udadavuzi makini zaidi. Mambo hayo ni
mafunzo ya matambiko na jamii ya waabudu wa Freemasons.
Hata
hivyo katika maelezo ya awali Sir Chande anasema chama hicho sio dini
na wala hakiingilii dini ya mtu, wala hakimkatazi mwanachama wake
kuabudu dini nyingine.
Uchunguzi wa Mpekuziblog
umebaini kuwa chapisho la Kiswahili la kitabu hicho lilizinduliwa
katika hafla kubwa iliyohudhuriwa na viongozi wakuu wanchi marais
wastafu, mabalozi na mgeni rasmi alikuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika
ukumbi wa shule ya Sekondari ya Shaaban Robert, Agosti 10, mwaka 2007.
BAADHI YA MANENO YA HOTUBA YA JK
Maneno yaliyopo kwenye hotuba ya Rais kikwete wakati wa uzinduzi wa kitabu hiki
yanadhihirisha upekee na umuhimu wake na hata kile kilichomo ambacho
wengi hawakijui. Rais katika sehemu ya hotuba hiyo alisema:
“….Aidha,
napenda kukupongeza kwa dhati kwa kitendo chako cha kuandika kitabu
hiki kinachohusu maisha yako. Sote tunatambua kuwa kuandika kitabu sio
kazi rahisi hata kidogo. Ni jambo linalohitaji ujasiri, umakini,
nidhamu na uwezo wa hali ya juu. Hivyo kwa kuandika kitabu hiki
kinachogusia maisha yako kwa kipindi kinachozidi miaka 77 umeonyesha
wazi kipaji na uwezo mkubwa ulio nao. Si watu wengi walio na uwezo kama
ulionao wewe. Tunakupongeza sana.
Lakini
kubwa zaidi nakupongeza kwa kuandika kitabu hiki kwa umakini na
ufasaha mkubwa. Umeweza kwa kiwango cha hali ya juu kueleza mazingira
halisi ya hali ya nchi yetu ulimokulia, kufanyia kazi na sasa
unamozeekea. Kitabu chako ni mchango mkubwa kwa historia ya nchi yetu
ambayo tunauenzi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Nawaomba
watanzania wenzangu wakisome kitabu hiki kila watakapopata nafasi,
ninahakika watafaidika sana na kile watakachokisoma. Ingekuwa jambo
jema sana maktaba za shule na vyuo vyetu vikawa na nakala ya kitabu
hiki, hivyo kuwawezesha vijana wetu kufahamu kwa undani zaidi historia
ya nchi yetu na watu wake kwa ujumla”
Rais Kikwete akiwa na kiongozi
mkuu wa mafreemason ,Sir Andy Chande
|
Lakini
hofu kubwa kwa jamii isiyofahamu vyema mambo hayo ni kuwepo kwa neno
kuabudu ambalo tafsiri rahisi ni Tafsiri hahisi ya Neno Matambiko
lililopo katika maelezo binafsi ya Sir Chande. Kwa mujibu wa kamusi ya
Kiswahili sanifu ni: Utekelezaji wa ada maalumu ili kutuliza mizimu, au
pepo, edah, kafara, mviga mviko.
Tafsiri
ya Neno kuabudu ni: “kufanya ibada, kuheshimu kwa hali ya juu
unyenyekevu wa hali ya ju. Aidha tafsiri nyingine zaidi ni tendo
linaloambatana na kutoa sadaka.
Akieleza safari yake jinsi alivyojiunga na kundi hilo Sir Chande alisema.
“Nilipoanza
kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambu kuwa nilikuwa
natumbukia katika mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na
dunia. Maana ingawa mpaka wakati huo Chama cha Freemason kilikuwa katika
sura hiyo hiyo kwa karibu miaka mia tatu (Kambi hizo mbili
ziliunganishwa uingereza mwaka 1715), hali ya usirisiri wake
unaokigubika imeongezeka sana katika miaka hii michache.
Freemason
walikuwako katika sehemu yangu hii ya dunia kwa muda wa miaka
hamsini, kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ikiwa imeanzishwa
Zanzibar mwaka 1904, lakini ikichukua miaka mingine ishirini na minne
kwa kambi ya kwanza ambayo, kwa shamra nyingi, Gavana ndiye
aliyeiwekea jiwe la msingi ili ijengwe huko Bara katika Mtaa ulioitwa
wakati ule; Main Avenue, sasa hivi Sokoine.
Post a Comment