STAA WA BONGO MOVE ATOA SINGO ‘KUMDISS’ NEY

Nyota kutoka tasnia ya filamu Bongo, Latifah Idabu ‘Badra’ ametoa ‘singo’  inayomchana  ‘live’ staa wa Bongo Fleva, Ney wa mitego (mbavu nene).

Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita  Badra amefunguka kuwa  ameamua kutengeneza ngoma hiyo kufuatia kauli chafu dhidi ya wasanii wa kike  aliyotowa Ney kwenye wimbo wake mpya wa hip hop  ujulikanao kama ‘Nasema nao’  unaotamba hivi sasa kwenye vituo mbalimbali  vya redio.

“Nimechukizwa mno na kitendo cha Ney kuimba kuwa  mastaa wa Bongo move ni makahaba , hawezi kusema hivyo na sisi tukaa kimya, ametushushia hadhi hasa ukizingatia sisi ni kioo cha jamii, ni zamu yake sasa  kusikia nilichomwambia na  kama kitamuuma  atajibu” alisema  Badra na kumalizia kwa tusi

Post a Comment

Previous Post Next Post