KAMATI ya Uchaguzi ya Klabu ya Yanga SC, jana ilipitisha majina
24 ya wagombea uongozi katika uchaguzi mdogo wa Julai 15, huku wagombea
wawili wakichujwa.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis
Kaswahili, wajumbe wawili waliochujwa kwa kushindwa kutokea kwenye
usaili, ni Abdallah Sharia na Jamal Kisongo.
Alisema waliopita kwa nafasi ya uenyekiti ni Yusuf Manji, Sarah
Ramadhan, John Jembele na Edgar Chibula huku Ayoub Nyenzi, Clement Sanga
na Yono Kevela wakipita kwenye nafasi ya makamu.
Waliopenya kwenye ujumbe, ni Lameck Nyambaya, Ramadhan Kampira,
Mohamed Mbaraka ‘Binkleb’, Ramadhan Saidi, Edgar Fongo, Ahmed Gao, Beda
Tindwa, Jumanne Mwammenywa na George Manyama.
Wengine ni Gadeuncius Ishengoma, Aaron Nyanda, Omary Ndula, Shaban Katwila, Justine Baruti, Peter Haule na Kevela.
Kaswahili alisema kampeni za wagombea, zitaanza Julai 3, kwa kila mmoja kunadi sera zake juu ya nini atafanya akishinda.
Katika hatua nyingine, usaili ulitawaliwa na vituko mbalimbali
vikiwemo vya baadhi ya wanachama kumlaki kwa shangwe mfadhili wao wa
zamani, Manji.
Manji aliyefika hapo kwa ajili ya kusailiwa, alijikuta akizingirwa na mamia ya watu waliokuwa wakiimba: “Rais..rais...rais!”
Uchaguzi huo unafanyika kuziba nafasi sita zilizoachwa wazi baada ya watano kujiuzulu kwa nyakati tofauti na mmoja kufariki.
Post a Comment