MASHINDANO
ya kumsaka mrembo wa Miss Universe Tanzania 2012 yatafanyika Ijumaa
hii kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yaliyopo Posta jijini Dar
es Salaam. Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Comm unications, Maria
Sarungi Tsehai amesema leo kuwa mashindano hayo yatawashirikisha jumla
ya warembo 20 kutoka katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.
Mikoa
hiyo ni Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Kilimanjaro na
wenyeji Dar es Salaam na kuongeza warembo wote wanaendelea na mazoezi
chini ya wakufunzi walioboea katika masuala ya urembo. “Tunatarajia
kuwa na mashindcano bora ili kuweza kumapata mrembo ambaye atatupa
sifa katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa Flaviana
Matata mwaka 2007 ambapo alishika nafasi ya saba katika mashindano
yaliyofanyika nchini Mexico,” alisema Maria.
Maria
aliwataja warembo hao kuwa ni Bahati Chando, Aisha Maulidi, Catherine
Mpulule, Cecilia Moses, Consolata Mosha, Devotha Keregese, Doris
Mollel, Doreen Mapunda na Edith Tesha. Wengine ni Getrude Asanterabi,
Jescha Tiba, Kundi Mligwa, Lilian Kolimba, Mary Joel, Naomi Joseph,
Nyaso Malilo, Neema Mpanda, Susan Manoko, Theodora Msenya na Winfrida
Dominic.
Alisema
kuwa shindano hilo limedhaminiwa na gazeti la The Citizen, gazeti
dada la Mwananchi kwa kushirikiana na wadhamini wengine, Le Grand
Casino, Urban Rose Hotel, Amina Design, Dodoma Hotel na New York Film
Academy.
Maria
alisema kuwa shindano hilo litaanza saa 1.00 usiku kwa warembo hao
kupita jukwaani wakiwa katika aina mbalimbali za mavazi kama vile ya
ubunifu na lile la usiku. Alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano
hilo kubwa la urembo yamekamilika na kinachosubiliwa ni siku ya
shindano hili kupata mrithi wa Miss Universe anayemaliza muda wake
Nelly Kamwelu.
Alifafanua
kuwa wameboresha mashindano ya mwaka huu na wanatarajia kuwa na
mashindano bora kabisa tofauti na ya miaka ya nyuma.
Post a Comment