Mohammed Mursi Aibuka Kidedea Uchaguzi Wa Misri
Mursi
ameshinda kura kwa asili mia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu
Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.
Mkuu
wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko
466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.
Tangazo
hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya
Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi wengi wa Bw.Mursi walikua
wamekuanyika.
Wafuasi
hao wamekaa kwenye medani hio kwa siku kadhaa wakionyesha msimamo wao
wa kuchukia sheria kadhaa zilizotangazwa na Baraza la juu la utawala wa
majeshi ambayo wanadai zimeundwa ili kupunguza mamlaka ya Rais na
kuelekeza uwezo mkubwa kwa majeshi.
Wafuasi
wa Bw.Shafiq nao waliweka kambi yao katika eneo la kaskazini mwa mji
ambako kuna makao makuu ya Tume ya uchaguzi huko Nasser City.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi Jaji Sultan alianza kwa kunena kua tangazo la
matokeo ya uchaguzi yalikua yamezongwa na shinikizo pamoja na hali ya
wasiwasi.
Tume
ya uchaguzi ilizingatia sheria ilipochunguza visanduku vya kupigia
kura, na Jaji.Sultan alisema hakuna kilicho juu ya sheria.
Jaji
huyo akaongezea kukanusha madai mawili nyeti kuhusu njama za kuibia
uchaguzi, kwamba baadhi ya karatasi za kupigia kura ziliwekwa ndani ya
visanduku tayari zikiwa na majina ya mgombea wanayemtaka ashinde.
Hatimaye
Jaji Sultan akamtangaza mshindi kua ni Bw.Mursi ambaye ni Mwenyekiti wa
chama cha Muslim Brotherhood cha Freedom and Justice, Bw.Mursi.
Baada
ya dakika kadhaa akitangaza marekebisho kuhusu matokeo madomadogo ya
kura ndipo akamtangaza Bw.Mursi kua mshindi kwa kuzoa kura 13,230,131,
na Bw.Shafiq akiweza kuzoa 12,347,380, sawa na asili mia 48.27%.
Chanzo: bbc swahili.
Post a Comment